Social Icons

Jumanne, 29 Julai 2014

MUONEKANO WA SASA WA UWANJA WA SIMBA SC

 


KATIKA historia yake, klabu ya Simba haijawahi kuwa na uwanja wake wa mazoezi, hivyo kujikuta anahangaika miaka nenda rudi.Lakini kwasasa unaweza kusema imedhamiria kujenga uwanja wa mazoezi maeneo ya Bunju jijini Dar es salaam.Ismail Aden Rage alipokaribia kumaliza muda wake alianza mchakato wa kujenga uwanja wa Bunju akisema wanataka kupata sehemu ya kufanyia mazoezi.Pia alisema wanakusudia kujenga hosteli za kuishi wachezaji ikiwa ni mkakati wa kupunguza gharama ya kuweka wachezaji hotelini.

Uongozi mpya chini ya Rais Evans Elieza Aveva alisema uko tayari kuendeleza ujenzi huo ulioanzishwa na Rage.

Mpaka sasa nyasi zilishapandwa na muonekano wa uwanja uko kama unavyoonekana pichani juu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates