Wananchi wakiwa wamejazana huku wakiliangalia lori aina ya fuso lililowagonga wafanyakazi sita wa kiwanda cha Mazava na mmoja kufariki dunia papo hapo kwa kuangukiwa na lori hilo baada ya kupinduka wakati dereva wake akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki katika barabara kuu ya Iringa-Morogoro eneo la Bene Msamvu mkoani Morogoro
Mkono ukiwa unanekana huku mwili ukiwa umekandamizwa na kichwa cha lori hilo kabla ya mwili kutolewa katika eneo la tukio.
Hapa mwili ukiwa bado haujatolewa.
Baada ya magari yenye kunyanyua vitu vizito kunyanyua na wananchi kupata nafasi ya kuutoa mwili uliokuwa umekandamizwa na lori hilo.
Hapa Kamanda Leonard Paul akizungumza na maafisa wake eneo la tukio.
Wapiga picha za facebook wakichukua picha.
Mfanyakazi kiwanda cha kushona jezi cha Mazava amefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebena kokoto kuacha njia na kupinduka kisha kuwafukia na kokoto hizo.
Mfanyakazi kiwanda cha kushona jezi cha Mazava amefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebena kokoto kuacha njia na kupinduka kisha kuwafukia na kokoto hizo.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 10:30 kwenye eneo la Bene Msamvu barabara ya Morogoro- Iringa na kwamba aliyefariki katika ajali hiyo ni Hanifa Bakari (20-30) ambaye ni mfanyakazi wa kiwanda hicho.
Ajali hiyo ilihusisha lori hilo aina ya Tiper lenye namba za usajili T 824 CVS lililokuwa likitokea Chamwino kwenda Msamvu na pikipiki aiana ya Honda yenye namba za usajili T823 CAE.
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Happines Santus (22), Anita Leonard (22), Shiza Ramadhani (23), Eliyas Banka, Adamu Mapande (18) na Fatuma Selemani (22) na mwanaume mmoja ambaye bado hajafahamika jina lake.
Akizungumza mara baada ya kuokolewa mmoja wa majeruhi hao Shiza Ramadhani alisema wakiwa wanatembea kandokando ya barabara ghafla walilioona lori hilo likiacha njia na kuwafuata upande waliokuwepo na kuwagonga kisha kufunikwa na kokoto.
Alisema kuwa kabla ya gari hilo kuwagonga alishuhudia pikipiki iliyokatiza ghafla mbele na dereva wa gari alipotaka kumkwepa ndipo aliacha njia na kwenda kuwagonga ambapo walitumbukia kwenye mtaro na kufukiwa na kokoto.
“Kama ingepita nusu saa bila ya kuokolewa kwa kweli ningekufa palepale kwa sababu tayari nilishaanza kuishiwa nguvu na kukosa hewa na sehemu kubwa ya mwili ilikuwa imefukiwa na kokoto,” alisema Shiza.
Hata hivyo baadhi ya watu waliofika kuwaokoa majeruhi hao walisema kuwa zana duni za uokoaji imekuwa ni tatizo kubwa mkoani hapa hivyo yanapotokea majanga ya aina hiyo vifo vimekuwa vikitokea kutokana na kuchelewa kwa zoezi la uokoaji.
Mmoja wa waokoaji hao Moris Masala alisema kuwa mara baada ya ajali hiyo kutokea kila mtu alikuwa hajui namna ya kuokoa majeruhi hivyo kwa gharama zake alilazimika kwenda kutafuta gari maalumu ya kunyanyau vitu vizito lakini ilishindwa kunyanyua gari hilo.
Moris alisema kuwa watu walianza kufukua kokoto hizo kwa kutumia zana duni za makoleo na hivyo kufanikiwa kuwatoa wafanyakazi hao sita na mmoja alitolewa akiwa tayari ameshafariki dunia.
Naye mbunge wa jimbo la Morogoro mjini AbdulAziz Abood alioneshwa kukerwa na tabia ya mmiliki wa kiwanda hicho ya kuwalazimisha wafanyakazi kutoka na kuingia kwa kutumia lango ambalo liko jirani na barabara kuu ya Morogoro- Iringa na hivyo kuhatarisha usalama wa wafanyakazi hasa wakati wa kuvuka barabara hiyo.
Hivyo alimtaka mmiliki huyo kufuata sheria na taratibu alizopewa kwani madhara ajali iliyotokea imesababisha kifo na majehara kwa wafanyakazi ambao ni watanzania.
Pia Abood alilitaka jeshi la polisi kuweka askari wa kudumu katika eneo hilo ambalo mara kadhaa ajali zimekuwa zikitokea na pia aliiomba wakara wa barabara nchini Tanroads kuweka matuta katika eneo hilo ili kudhibiti mwendokasi wa maredeva.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani hapa Leonard Paulo alikiri eneo hilo kuwa hatarishi na hivyo kuahidi kuweka askari wa usalama barabarani ambao watakaa muda wote kudhibiti mwendo kasi ili kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara katika eneo hilo.
Alisema kuwa tayari dereva wa gari lillilosababisha ajali Ayubu Swai (27) na dereva wa Pikipiki Samwel Noel (32) wameshakamatwa kwa mahojiano zaidi na watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa polisi kukamilika.
Hata hivyo alisema majeruhi waliolazwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro wanaendelea vizuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni