Dili limekamilika: Jana jumatano, Lukaku alitambulishwa na kocha wake wa Everton, Roberto Martinez.
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho alimpiga dongo Romelu Lukaku jana usiku baada ya kukamilisha uhamisho wa paundi milioni 28 kujiunga na Everton.Lukaku alijiunga na Chelsea msimu mitatu iliyopita, lakini alicheza mechi 10 tu za ligi kuu kabla ya kutolewa kwa mkopo katika klabu West Brom na baadaye Everton.Akizungumza baada ya ushindi wa mabao 3-1 iliopata Chelsea kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Vitesse Arnhem, Mourinho, alisema nyota huyo mwenye miaka 21 hakuandaliwa kushindania nafasi ya kucheza klabuni.
Tabasamu: Mshambuliaji huyo wa Everton alifurahia kurudi Goodison Park
Madongo kama kawaida: Mourinho (kulia) akitazama timu yake ya Chelsea iliyoitandika Vitesse mabao 3-1 jana jumatano.
Alisema: 'Ukweli ni kwamba Romelu alikuwa wazi kwetu kwamba akili yake haikuwa tayari na hakuwa na morali ya kuja kupambana kutafuta namba katika kikosi cha Chelsea".
"Alitaka kuichezea Chelsea, lakini alihitaji kuwa mshambuliaji chaguo la kwanza, kitu ambacho ni kigumu kwa klabu yetu hasa kwa aina ya mchezaji kama yeye. Alipunguza hamu ya kuja kwetu".
Mourinho alisisitiza kuwa hana tatizo na Lukaku: "Kitu cha msingi ni kwamba ana furaha na anafanya kazi vizuri, ni mtoto mzuri na ana namna yake ya kuwaza mambo yake".
"Yote kwa yote, namtakia kila la kheri. Anastahili bahati na kuwa na furaha".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni