Social Icons

Alhamisi, 31 Julai 2014

MARAIS WASTAAFU THABO MBEKI, FESTUS MOGAE NA BENJAMIN MKAPA WAKUTANA DAR ES SALAAM

1a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Festus Mogae wa Botswana wakiigia kwenye chumba cha Mkutano katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa Africa Readership Forum ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es salaam ambao ulikuwa unajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi za Afrika na kuangalia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za kushughulikia changamoto hizo.
2a
Rais mstaafu wa wa Afrika Kusin Thabo Mbeki akizungumza katika mkutano huo uliojumuisha viongozi mbalimbali wa afrika na taasisi mbalimbali kweye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
3a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini katikati ,Festus Mogae wa Botswana kushoo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa wakiwa wakiongoza mkutano huo.
4a
Baadhi ya viongozi kutoka taasisi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.
5a
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe katikati ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katik mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
6a
Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye kulia ni Mh. Balozi Ali Karume walikuwa ni miogoni wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo pia.

MAGAZETI YA LEO


1_7d8ae.jpg
25_5550b.jpg
2_fc8c2.jpg
24_7c4c1.jpg
04_c8353.jpg
28_9bd24.jpg
3_9c34f.jpg

028_71f9f.jpg
4_0867b.jpg

29_b1e22.jpg
5_19191.jpg

26_b1b8a.jpg6_19e5d.jpg
27_20106.jpg7_30af0.jpg

030_9ae2c.jpg
08_cb39a.jpg
9_fdc89.jpg
30_0e8a5.jpg
10_37eb5.jpg
32_444f2.jpg31_a1ba5.jpg

LIVERPOOL YAINYUKA MANCHESTER CITY CITY KWA PENALTI 3-1 NEW YORK

Smothered:  Joe Hart makes a save from Philippe Coutinho during the New York friendly


 Joe Hart akiokoa mpira uliopigwa na Philippe Coutinho wakati wa mechi ya kirafiki mjini New York 
MAJOGOO wa jiji, Liverpool waliwalaza mabingwa wa England, Manchester City kwa penalti 3-1  kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 za mchezo wa Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya Uwanja wa Yankee, nchini Marekani. 
Mabao ya kikosi cha Brendan Rodgers yalifungwa na Jordan Henderson katika dakika ya 59 na kinda Raheem Sterling mnamo dakika ya 85.
Magoli ya Man City inayonolewa na kocha raia wa Chile, Manuel Pellegrini yalifungwa na  Stevan Jovetic dakika za 53 na 67 .
Wakati wa upigaji wa Mikwaju ya penalti Yaya Toure na Jesus Navas walishindwa kuzamisha mpira nyavuni baada ya kuokolewa na  Mignolet, wakati huo huo Aleksandar Kolarov naye alikosa - hivyo kumpa nafasi Lucas Leiva kuipa ushindi wa 3-1 timu ya Liverpool. Penati pekee ya Man City ilifungwa Iheanacho.
Sturridge pia alipaisha penalti yake, lakini Emre Can na Henderson walifunga kabla ya Lucas kutumbukiza penalti nyavuni.
Timu hiyo ya Merseysiders sasa itachuana na AC Milan mjini Charlotte Jumamosi ikiwa na nafasi ya kuongoza kundi lake- ili ikutane na mahasimu, Manchester United inayofundishwa na Louis van Gaal mjini Miami.
Red sea: Liverpool fans pack inside the Yankee Stadium in New York
Mashabiki wa Liverpool walifurika uwanja wa  Yankee mjini New York.

Kikosi cha Liverpool: Jones, Kelly (Johnson 46), Toure, Coates (Sakho 76), Enrique (Robinson 46), Gerrard (Lucas 76), Henderson, Allen (Can 65), Coutinho, Lambert (Sterling 46), Sturridge. 
Wachezaji wa akiba : Mignolet, Ward, Suso, Ibe, Coady, Peterson.
Wafungaji wa magoli: Henderson 59, Sterling 85.

Kikosi cha Manchester City: Caballero (Hart 46), Clichy (Richards 70), Kolarov, Boyata, Nastasic, Fernando, Navas, Zuculini, Milner (Sinclair 46), Jovetic (Yaya Toure 70), Dzeko (Iheanacho 46). 
Wachezaji wa akiba: Nasri, Negredo, Garcia, Rodwell, Rekik, Silva, Wright, Lawlor, Huws, Guidetti, Bossaerts, Denayer.
Mfunagiji wa mabao: Jovetic 53, 67.
On the move: City's Edin Dzeko tries to take on Coates
Nyota wa Man City Edin Dzeko akijaribu kumtoka mchezaji wa Liverpool

MOURINHO AMTANDIKA `BAKORA` ROMELU LUKAKU BAADA YA KUHAMIA EVERTON

Done deal: Lukaku is unveiled at Everton on Wednesday alongside manager Roberto Martinez
Dili limekamilika: Jana jumatano, Lukaku alitambulishwa na  kocha wake wa Everton, Roberto Martinez.
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho alimpiga dongo  Romelu Lukaku jana usiku baada ya kukamilisha uhamisho wa paundi milioni 28 kujiunga na Everton.Lukaku alijiunga na Chelsea msimu mitatu iliyopita, lakini alicheza mechi 10 tu za ligi kuu kabla ya kutolewa kwa mkopo katika klabu West Brom na baadaye Everton.Akizungumza baada ya ushindi wa mabao 3-1 iliopata Chelsea kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya  Vitesse Arnhem, Mourinho, alisema nyota huyo mwenye miaka 21 hakuandaliwa kushindania nafasi ya kucheza klabuni.
Smiles better: The Belgian striker expressed his delight at returning to Goodison Park
Tabasamu: Mshambuliaji huyo wa Everton alifurahia kurudi Goodison Park 
Parting shot: Mourinho (right) watches from the touchline as Chelsea beat Vitesse 3-1 on Wednesday
Madongo kama kawaida: Mourinho (kulia) akitazama timu yake ya Chelsea iliyoitandika Vitesse  mabao 3-1 jana jumatano.

    Alisema: 'Ukweli ni kwamba Romelu alikuwa wazi kwetu kwamba akili yake haikuwa tayari na hakuwa na morali ya kuja kupambana kutafuta namba katika kikosi cha Chelsea".

    "Alitaka kuichezea Chelsea, lakini alihitaji kuwa mshambuliaji chaguo la kwanza, kitu ambacho ni kigumu kwa klabu yetu hasa kwa aina ya mchezaji kama yeye. Alipunguza hamu ya kuja kwetu".
    Mourinho alisisitiza kuwa hana tatizo na Lukaku: "Kitu cha msingi ni kwamba ana furaha na anafanya kazi vizuri, ni mtoto mzuri na ana namna yake ya kuwaza mambo yake".
    "Yote kwa yote, namtakia kila la kheri. Anastahili bahati na kuwa na furaha".

    WATU WANNE WAMEFARIKI PAPO HAPO BAADA YA KUDONDOKEWA NA KUFUNIKWA NA LORI LA MIZIGO

     Lori hilo la mizigo likiwa limedondoka Chini ya Mto njia panda ya Ilembula huku  watu wanne wakiwa wamefunikwa.
    Watu wanne wamefariki papo hapo Saa kumi usiku leo baada ya kudondokewa na Lori la mizigo , Lililopindukia katika mto njia panda ya kuelekea Ilembula, kutokana na kufunikwa na Lori hilo watu hao wameendelea kuwa chini ya Lori hilo na Kazi ya kuwatoa inaendelea kufanyika sasa.

     Baadhi ya watu wakiwa wanashuhudia tukio la ajali huku wengine wakijipanga jinsi ya kuwaokoa walifunikwa na kifusi.
     Baadhi ya mizigo ikiwa imedondoka katika mto
     Hivi ndivyo Lori linavyo onekana likiwa limedondoka chini ya mto eneo la njiapanda Ilembula
     Mashuhuda wakiwa wanaongezeka kufika katika eneo la Tukio

     Kazi ya uokoaji ikiwa imeanza 
     Lori la mizigo likiwa limedondoka

    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WAKIHUSISHWA NA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI MKOANI ARUSHA

    LiberatusSabas
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
    WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
    JESHI LA POLISI TANZANIA
     
    NDUGU WANAHABARI, MTAKUMBUKA KUWA WIKI MOJA ILIYOPITA JESHI LA POLISI LILITOA TAARIFA KWA UMMA JUU YA WATUHUMIWA SITA WALIOKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KUHUSIANA NA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA TAREHE 07/07/2014 KATIKA MGAHAWA WA VAMA ULIOPO MAENEO YA VIWANJA VYA GYMKANA JIJINI ARUSHA.
    TAARIFA HIYO ILIZUNGUMZIA PIA TUKIO LA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE BAADA YA KUPEKULIWA NYUMBANI KWAKE ALIKUTWA NA MABOMU SABA YA KURUSHA KWA MKONO, RISASI SITA ZA BUNDUKI AINA YA SHOT-GUN PAMOJA NA UNGA WA BARUTI. TULIELEZA PIA KUWA OPERESHENI YA KUKAMATA WATUHUMIWA WENGINE KUHUSIANA NA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI ILIKUWA IKIENDELEA, NA KWAMBA WATUHUMIWA KADHAA WALIKUWA CHINI YA ULINZI WA POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO HAYO.
    KUTOKANA NA OPERESHENI HIYO ENDELEVU, WATUHUMIWA WENGINE KADHAA WAMEKWISHA KAMATWA NA KUHOJIWA, AMBAPO USHAHIDI ULIOKUSANYWA UMEBAINI KUWA  KATI YAO  WATUHUMIWA ISHIRINI NA MOJA (21) WANAHUSIKA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI YA ULIPUAJI MABOMU NA KUMWAGIA WATU TINDIKALI HAPA JIJINI ARUSHA KATIKA KIPINDI CHA KUANZIA MWAKA 2012 HADI YALE YALIYOTOKEA KATIKA KIPINDI CHA HIVI KARIBUNI. WATUHUMIWA HAO WANATAZAMIWA KUFIKISHWA MAHAKAMANI TAREHE 01/08/2014 KUUNGANA NA WENZAO WALIOKWISHA TANGULIA ILI KUJIBU MASHITAKA YANAYOWAKABILI. UFAFANUZI WA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA NA MATUKIO WALIYOHUSIKA NAYO NI KAMA IFUATAVYO:
    I.             TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU NYUMBANI KWA SHEKH ABDULKARIM JONJO  TAREHE 25/10/2012
    WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
    1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO
     
    2.    KASSIM S/O IDRISA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNERLL
     
    3.    MUSTAPHA S/O MOHAMED KIAGO, MZIGUA, MIAKA 49, MKAZI WA KALOLENI, NI SHEKH MSIKITI MKUU WA IJUMA
     
    4.    ABDUL-AZIZ S/O MOHAMED, MCHAGA, MIAKA 49, MKAZI WA ENEO LA FAYA, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI MKUU WA IJUMAA
     
    II.          TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA ST. JOSEPH MFANYAKAZI OLASITI LA TAREHE 05/05/2013
    WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
    1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO.
     
    2.    RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO.
     
    3.    ABDUL S/O MOHAMED HUMUD @ WAGOBA, MMANYEMA, MIAKA 30, MKAZI WA MURIET, WAKALA WA MABASI YA MOHAMED TRANS (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
     
    4.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
     
    5.    SAID S/O  MICHAEL TEMBA, MCHAGA, MIAKA 42, MKAZI WA SINONI- UNGA LTD, MFANYABIASHARA SOKO LA KILOMBERO (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
     
    6.    KASSIM S/O IDRISA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER
    7.    ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA
    8.    ABDULRAHAMAN S/O JUMANNE HASSAN, MBONDEI, MIAKA 41, MKAZI WA SINONI, MFANYAKAZI WA STANBIC BANK ARUSHA
     
    9.    MORRIS S/O JOHN MUZI, MUHA, MIAKA 44, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
     
    10. NIGANYA S/O HAMISI NIGANYA, MUHA, MIAKA 28, MKAZI WA BUSINDE UJIJI MKOANI KIGOMA
     
    11. BARAKA S/O NTEMBO BILANGO, MUHA, MIAKA 40, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
     
    12. HASSAN S/O ABDALLAH OMAR, MNYATURU, MIAKA 40, MKAZI WA ILONGERO MKOANI SINGIDA
     
     
    III.        TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU VIWANJA VYA SOWETO KWENYE MKUTANO WA CHADEMA TAREHE 15/06/2013
    WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
    1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO
     
    2.    ABDUL S/O MOHAMED HUMUD @ WAGOBA, MMANYEMA, MIAKA 30, MKAZI WA MURIET, WAKALA WA MABASI YA MOHAMED TRANS (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
     
    3.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
     
    4.    SAID S/O  MICHAEL TEMBA, MCHAGA, MIAKA 42, MKAZI WA SINONI- UNGA LTD, MFANYABIASHARA SOKO LA KILOMBERO (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
    5.    KASSIM S/O IDRISSA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER
     
    6.    RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO
     
    7.    ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA
     
    8.    ABDULRAHAMAN S/O JUMANNE HASSAN, MBONDEI, MIAKA 41, MKAZI WA SINONI, MFANYAKAZI WA STANBIC BANK ARUSHA
    9.    MORRIS S/O JOHN MUZI, MUHA, MIAKA 44, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
     
    10. NIGANYA S/O HAMISI NIGANYA, MUHA, MIAKA 28, MKAZI WA BUSINDE UJIJI MKOANI KIGOMA
    11. BARAKA S/O NTEMBO BILANGO, MUHA, MIAKA 40, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
     
    12. HASSAN S/O ABDALLAH OMAR, MNYATURU, MIAKA 40, MKAZI WA ILONGERO MKOANI SINGIDA
     
    IV.          TUKIO LA KUMWAGIWA TINDIKALI SHEKH SAID JUMA MAKAMBA WA MSIKITI WA KWA MOROMBO TAREHE 11/07/2013
    WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
    1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO
     
    2.    RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO.
     
    3.    KASSIM S/O IDRISA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER
     
    4.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
     
    V.           TUKIO LA KUMWAGIWA TINDIKALI SHEKH MUSTAPHA KIAGO WA MSIKITI MKUU LA TAREHE 28/02/2014
    WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
    1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO
     
    2.    KASSIM S/O IDRISSA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER
     
    3.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
     
    4.    HASSAN S/O ALLY MFINANGA, MPARE, MIAKA 57, MKAZI WA MAKAO MAPYA, BIASHARA
     
    VI.          TUKIO LA BOMU ARUSHA NIGHT PARK (MTK) LA TAREHE 13/04/2014
    WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
    1.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
     
    2.    IBRAHIM S/O LENARD @ SHEKH ABUU ISMAIL, MSUKUMA, MIAKA 37, MKAZI WA MABATINI MKOANI MWANZA.
     
    VII.      TUKIO LA BOMU NYUMBANI KWA SHEKH SUDI ALLY SUDI LA TAREHE 03/07/2014
    WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
    1.    YAHAYA S/O TWALIB TWAHIR @ MPEMBA, MSAMBAA, MIAKA 37, MKAZI WA MTAA WA JALUO, MFANYABIASHARA YA DUKA MTAA WA BONDENI
     
    2.    IDD S/O RAMADHAN YUSUPH, MSAMBAA, MIAKA 23, MKAZI WA MTAA WA JALUO.
     
    3.    SAID S/O  MICHAEL TEMBA, MCHAGA, MIAKA 42, MKAZI WA SINONI- UNGA LTD, MFANYABIASHARA SOKO LA KILOMBERO (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWAWA VAMA)
     
    4.    ANWAR S/O NASHER HAYEL, MNYAMWEZI, MIAKA 29, MKAZI WA  NGULELO, MFANYABIASHARA
     
    5.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
    6.    HASSAN S/O ALLY MFINANGA, MPARE, MIAKA 57, MKAZI WA MAKAO MAPYA, BIASHARA
     
    7.    YUSUPH S/O ALLY RAADHAN @ SEFU, MPARE, MIAKA 23, MKAZI WA NGUSERO
     
    8.    ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA
    VIII.    TUKIO LA KUPATIKANA NA MABOMU LA TAREHE 21/07/2014
    WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
    1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO
     
    2.    SUMAIYA W/O YUSUPH HUSEIN ALLY, MWASI, MIAKA 19, MKAZI WA NGUSERO.
     
    3.    RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO.
     
    4.    HASSAN S/O ALLY MFINANGA, MPARE, MIAKA 57, MKAZI WA MAKAO MAPYA, BIASHARA
     
    5.    ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA
     
    6.    KIMORO S/O ISSA MCHANA @  OMAR @ ABUU TWALIB, MRANGI, 25YRS, MKAZI WA ITOLWA KONDOA
     
    7.    HASSAN S/O ABDALLAH OMAR, MNYATURU, MIAKA 40, MKAZI WA ILONGERO MKOANI SINGIDA.
     
    8.    MORRIS S/O JOHN MUZI, MUHA, MIAKA 44, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
     
    9.    NIGANYA S/O HAMISI NIGANYA, MUHA, MIAKA 28, MKAZI WA BUSINDE UJIJI MKOANI KIGOMA
    10. BARAKA S/O NTEMBO BILANGO, MUHA, MIAKA 40, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
    IX.          KOSA LA KUHAMASISHA VITENDO VYA KIGAIDI KUPITIA MTANDAO WA KIJAMII
    WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
    1.    IBRAHIM S/O LENARD @ SHEKH ABUU ISMAIL, MSUKUMA, MIAKA 37, MKAZI WA MABATINI MKOANI MWANZA.
    2.    ANWAR S/O NASHER HAYEL, MNYAMWEZI, MIAKA 29, MKAZI WA  NGULELO, MFANYABIASHARA
    3.    YASINI S/O MOHAMED SHABAN @ YAKI, MCHAGA, MIAKA 20, MKAZI WA KALOLENI MITA 200
    OPERESHENI YA  KUWATAFUTA WATUHUMIWA WENGINE WA MATUKIO HAYA INAENDELEA NCHI NZIMA, NA TAYARI TUNAYO MAJINA YA WATUHUMIWA KADHAA AMBAO WAMETOWEKA ARUSHA NA KUELEKEA MAENEO MBALIMBALI YA NDANI NA NJE YA NCHI. MTUHUMIWA MMOJAWAPO ANAYETAFUTWA SANA NA POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO HAYA NI YAHAYA HASSAN HELLA @ SENSEI, KABILA NI MRANGI, MZALIWA WA KIJIJI CHA CHEMCHEM WILAYA YA KONDOA.
    IMEBAINIKA KUWA MTUHUMIWA HUYO NDIYE KINARA WA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI HAPA JIJINI ARUSHA KWA KUSHIRIKIANA NA WENZAKE WALIOKAMATWA, NA AMBAO BADO WANAENDELEA KUTAFUTWA. JESHI LA POLISI  LINAFANYA KILA JITIHADA KUWEZA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WOTE WALIOTOROKA NA KUHAKIKISHA KUWA SHERIA INACHUKUA MKONDO WAKE.
    ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
    IMETOLEWA NA:-
     
     
    LIBERATUS M. SABAS – SACP
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
     
     
    Blogger Templates