Social Icons

Jumatatu, 2 Juni 2014

Wachunguzi kukutana na maafisa Qatar

Uwanja ambao umepangiwa michuano ya kombe la dunia 2022 Qatar

Jumapili, gazeti la SUNDAY TIMES la Uingereza, liliripoti kwamba mamilioni ya pauni zilitolewa kama malipo kwa maafisa waliounga mkono ombi la Qatar kuandaa michuano hiyo mwaka 2022, tuhuma ambazo Qatar imepinga vikali.

Fifa imesema ombi jipya linapaswa kuruhusiwa iwapo tuhuma hizo za rushwa zitathibitishwa. Makamu wa Rais wa Fifa, Jim Boyce, anasema kuwa ataunga mkono hatua ya kupiga kura tena ikiwa madai hayo yatathibitishwa ili kuteua nchi nyingine.


Afisaa mmoja wa kamati ya FIFA, Lord Goldsmith, alisema kuwa ''Ikiwa itathibitishwa kuwa uamuzi wa kuipa Qatar idhini ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2022 ulitokana na hongo kulipwa maafisa wa shirikisho la FIFA, basi uamuzi wa kuinyima nchi hiyo haki hiyo lazima uchukuliwe. ''
Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa FA Mark Palios, anadhani kwamba rais wa FIFA Sepp Blatter anajitahidi kulinda kazi yake.
Garcia anatarajiwa kukutana na maafisa wa FIFA nchini Qatar. Wakili huyo anachunguza madai mengine ya tuhumza dhidi ya maafisa wa FIFA kuhusiana na kombe la dunia mwaka 2018 na 2022.
Jarida la Sunday Times, linadai kuwa maafisa wa soka walipokea hongo ya kima cha pauni milioni 3 ili waweze kuunga mkono azma ya Qatar kutaka kuandaa kombe la dunia mwaka 2022.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates