Benoit Assou-Ekotto akimtwanga 'ndoo' Moukandjo.
Benoit Assou-Ekotto (kulia) akimsogelea mwenzake Benjamin Moukandjo baada ya kipigo cha 4-0 kutoka kwa Croatia usiku wa kuamkia leo.
Moukandjo akimjia juu Ekotto baada ya kichwa hicho.
Samuel Eto'o akimtuliza Ekotto aliyepandisha hasira baada ya kichapo cha 4-0.
BEKI wa Cameroon, Benoit Assou-Ekotto aliamua kumpiga kichwa 'ndoo' mchezaji mwenzake Benjamin Moukandjo kufuatia kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Croatia.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo wakati wa mechi ya Kombe la Dunia 2014 kati ya Cameroon na Croatia.
Katika mpambano huo Cameroon waliambulia kichapo cha mabao 4-0 na kuyaaga mashindano hayo baada ya kupoteza pia mechi yao ya kwanza dhidi ya Mexico kwa bao 1-0.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni