Social Icons

Ijumaa, 20 Juni 2014

SEHEMU YA BARABARA YA UBUNGO MATAA DAR ES SALAAM KUFUNGWA KESHO NA KESHOKUTWA USIKU KUPISHA UJENZI WA BARABARA


KAMPUNI ya ujenzi ya Strabag International GmbH inayojenga barabara ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) imetangaza mabadiliko ya muda katika eneo la Ubungo jijini Dar es salaam kuanzia kesho na kesho kutwa usiku kutokana na ujenzi unaoendelea wa barabara.
Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Bwana Yahya Mkumba, alisema  kazi hiyo itahusu ujenzi katika makutano ya barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Nelson Mandela katika eneo la Ubungo.
Alisema ujenzi huo utakaoanza leo utasababisha kufungwa kwa baadhi ya njia katika barabara hizo kuanzia saa nne usiku hadi saa 12 asubuhi kesho Jumamosi.
Akielezea zaidi alisema katika awamu ya kwanza ujenzi huo utahusisha eneo la upande wa kulia la makutano la barabara ya Sam Nujoma na Morogoro ambalo litafungwa.
“Hali hii itasababisha magari yanayotoka maeneo ya Buguruni na Tabata kuelekea maeneo ya Mwenge kutoweza kutumia njia ya Sam Nujoma watakapofika taa za Ubungo,” alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates