Social Icons

Jumatano, 11 Juni 2014

BULEMBO AMPONDA MBATIA, ASEMA HANA SHUKRANI.

JAMES MBATI BAADA YA KUTEULIWA KUWA MBUNGE
MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi  ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdalla Bullembo amemnanga Mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia akidai kwamba hana shukrani.

Bulembo amesema kabla ya kuteuliwa, Mbatia alikuwa na maisha magumu lakini baada ya kuteuliwa mambo yake yalianza kubadilika na kurudisha hadhi yake katika jamii.

Hivi sasa ana gari zuri, anava vizuri na kupendeza , anakula vizuri huku akijivunia uheshimiwa unaotokana na hekima za Rais Jakaya Kikwete aliyemteua kupitia nafasi zake kumi za uteuzi wa wabunge.


Pamoja na hayo yote, Bulembo amesema Mbatia amekosa shukrani kwa kitendo chake cha kujiunga na UKAWA na kupanda majukwani kuiponda serikali ya CCM iliyompa ulaji

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates