Social Icons

Jumatano, 11 Juni 2014

MUFTI WA TANZANIA SHAABAN SIMBA AONGOZA BAADHI YA WAISLAM KUVUNJA MILANGO YA MSIKITI MKUU WA IJUMAA TABORA


Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu msikiti mkuu wa Ijumaa Gongoni mjini Tabora wakati wa tukio la kuvunjwa milango ya msikiti huo unaodaiwa kufungwa na baadhi ya viongozi walioondolewa madarakani na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Simba kwa madai ya kukiuka utaratibu wa Baraza kuu la Waislam Tanzania Bakwata,ambapo Mufti aliongoza tukio la kuvunja milango ya msikiti huo jambo ambalo lilipingwa vikali na baadhi ya waumini wanaowaungamkono viongozi waliosimamishwa akiwemo Sheikh mkuu wa mkoa wa Tabora Shaban Salum.
Mara baada ya kuvunjwa kwa msikiti huo huku kukiwa na ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi Mufti Shaban Simba aliingia ndani na kuzungumza na baadhi ya waumini ambapo aliendelea na msimamo wa kumsimamisha Sheikh wa mkoa wa Tabora Shaban Salum hatua ambayo imeendelea kulalamikiwa na idadi kubwa ya waumini wa dini ya kiislam hasa wanaofanya ibada katika msikiti huo wa Ijumaa.
Mufti Shaaban Issa Simba akiwa ndani ya msikiti wa Ijumaa baada ya kuvunjwa licha ya kuwa katika milango ya msikiti huo kulikuwa na hati ya mahakama ya kulalamikiwa kwa Mufti huyo.
Baadhi ya waumini nje ya msikiti walikuwa wakihojiwa na waandishi wa habari ambapo wameendelea kumlalamikia kiongozi huyo mkubwa wa waislam nchini kwa hatua ya kumsimamisha Sheikh wa mkoa wa Tabora jambo ambalo wamedai kuwa ni moja ya hatua ya kuidhalilisha dini ya kiislam kwakuwa suala hilo lingetafutiwa ufumbuzi kwa vikao vya ndani na kwakuzingatia busara zaidi kuliko hali ilivyokuwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates