Shambulizi jingine limetokea katika eneo la Mpeketoni karibu na Lamu , pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu 10.
Shambulizi la leo limetokea siku moja tu baada ya Al Shabaab kukiri kufanya mashambulizi yaliyowaua watu 50 Jumatatu.
Polisi wanasema kuwa washambuiaji hao walivamia kijiji kimoja usiku kucha.
Kundi la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo na kuambia shirika la Reuters kuwa operesheni yao ya mashambulizi itaendelea nchini Kenya.
Takriban watu 50 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni