Social Icons

Jumapili, 29 Juni 2014

Dk Salim apongezwa


“Ni vizuri viongozi wakaandaliwa, isiwe mtu anaibuka tu anagawa hela halafu anashinda. Anatakiwa mtu atakayeweza kushughulikia matatizo ya Watanzania. Watanzania ni wapole na wavumilivu lakini wanazungumza. Hivyo anahitajika kiongozi atakayesikiliza mahitaji yao na kutoa suluhisho, si kutoa ahadi za uongo,” Dk Salim Ahmed Salim Kwa ufupi
  • Wakizungumza na gazeti hili wamesema, Dk Salim ametambua mchango alioutoa kwa taifa hivyo hana budi kuwaachia nafasi vijana nao wakatawala.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Waziri Mkuu mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim kusema kuwa hana mpango na hafikirii tena kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, wasomi na wanasiasa wamezungumzia kauli hiyo wakisema ni ya kishujaa inayofaa kuigwa na viongozi  wengine.Wakizungumza na gazeti hili wamesema, Dk Salim ametambua mchango alioutoa kwa taifa hivyo hana budi kuwaachia nafasi vijana nao wakatawala.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema Dk Salim hana anachotaka kukifanya kwani amelitumikia taifa kwa kipindi kirefu hivyo ameona ni busara kujiweka kando na kuwa mshauri.“Ni kauli nzuri na inayoheshimu busara, nafasi za uongozi alizofikia ni hakika zinatosha kulingana na umri wake na siasa chafu za nchini ni bora akawa pembeni na akatumika kama mshauri tu,” alisema Dk Bana.Naye mtaalamu wa masuala ya maendeleo na siasa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Idd Makombe  alisema Dk Salim amejifunza kutokana na  siasa za mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu zilivyochafuliwa.Alisema Dk Salim ameona bora ajiondoe kulinda heshima yake, kitendo kinachotakiwa kuigwa na wanasiasa wengine.“Mimi ninaamini kuwa kama Dk Salim angesimama katika uchaguzi uliopita au ujao na kusiwepo na siasa chafu, angeshinda bila ubishi,” alisema Dk Makombe.Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema kitendo cha Dk Salim kueleza kuwa ni lazima kuwa na sifa za ziada ndiyo ushinde, imedhihirisha jinsi CCM inavyowapata viongozi wake kwa njia zisizostahili.“Hata uwe na sifa za aina gani lakini lazima ufanye ujanja ujanja ndiyo ushinde. Sasa kwa watu ambao hawawezi kutumia mbinu hizo ndiyo kama Dk Salim, anaona bora akae kando kwani haziwezi mbinu hizo,” alisema Nyambabe.Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema, Dk Salim anatakiwa kuandika kitabu kuelezea yaliyojiri tangu awamu ya kwanza ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere hadi awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa katika mchakato wa kumpata mgombea urais.Alisema kutokana na kuwa na uzoefu wa kimataifa alimshauri Dk Salim atumie kitabu hicho kuelezea uzoefu wa mataifa mengine kuwapata wagombea urais unavyokuwa akifananisha na chama chake CCM ili kiwe ngazi na  tunu ya taifa kwa kizazi kijacho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates