Social Icons

Jumatatu, 9 Juni 2014

Jimmy Mack, alipoteza maisha,Hali ya Mchekeshaji Tracy Morgan ni mbaya sana .

Mchekeshaji maarufu wa nchini Marekani Tracy Morgan bado yupo katika hali mbaya kiafya kutokana na ajali mbaya ya gari aliyopata mwishoni mwa wiki.

Muigizaji huyo wa vichekesho anakabiliwa na majeraha ya kuvunjika mbavu, pua na mguu baada ya gari aliyokuwa akisafiria kugongwa na gari kubwa na kusababisha ajali mbaya.
Baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake, Morgan ameanza kuonyesha matumaini lakini ataendelea kubaki hospitalini kwa wiki kadhaa akipatiwa matibabu, kwa mujibu wa msemaji wake.
tracy2
Katika ajali hiyo iliyotokea mjini New Jersey muigizaji mwingine wa vichekesho Jimmy Mack, alipoteza maisha.

huyo happ chini ndio Jimmy Mack.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates