Mamlaka nchini Saudia Arabia ipo kwenye zoezi la kupima chokleti za Cadbury zinazotengenezwa Uingereza kufuatia kashfa juu ya kuwekwa kwa
virutubisho vya nyama ya nguruwe kwenye bidhaa hizo kugunduliwa nchini Malaysia ambapo wito wa mgomo uliotolewa kwa makampuni yanayodhalisha bidhaa hiyo.
Siku chache zilizopita Mamlaka nchini Malaysia iligundua uwepo wa nyama za nguruwe kwa kutumia DNA katika bidhaa hiyo ya Cardbury Daily Milk huku taarifa ikimnukuu makamu wa Rais wa sekta ya Chakula(SFDA) akisema kwamba kufanya vipimo hakukuhusisha bidhaa nyingine za Cardbury zinazozalishwa katika viwanda vya Malaysia na zilikuwa zikiagizwa kutoka nchi nyingine kama vile Misri na Uingereza.
Ijumaa iliyopita Taifa la Indonesia lenye wakazi wengi waislamu nao pia walikuwa wakipima bidhaa hizo kwa kuangalia kama zinazingatia vigezo vya kiislamu. Kashfa ya masharika yanayotengeneza vyakula visivyo halali ilianzia kusini mwa bara la Asia ambapo mwaka 2001 baraza la maulamaa la nchini Indonesia liliishtaki kampuni kubwa ya kijapani Ajinimoto iliyokuwa inatengeneza bidhaa za kula kwa kutumia virutubisho vya nyama ya nguruwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni