Social Icons

Jumanne, 24 Juni 2014

AGIZO: Mikutano ya Nape yapigwa ‘stop’

Mtwara. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ameonja chungu ya uamuzi wa Serikali wa kusitisha mikutano ya hadhara katika mikoa ya Lindi na Mtwara baada ya kushindwa kufungua mashina ya chama hicho mjini Mtwara.
Nape ambaye alikuwa mkoani Mtwara kwa ziara ya siku moja, alijikuta akiishia kuwakabidhi bendera za chama hicho viongozi wa matawi ili wakazipandishe wenyewe kimyakimya.
Akizungumzia hatua hiyo, Nape alisema amri hiyo ya kusitisha mikutano imekuwa kikwazo na inadidimiza demokrasia katika mikoa hiyo, hivyo Serikali inapaswa kuibadili ili kuruhusu iendelee kufanyika. Mashina ya chama hicho ambayo yalitarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki ni Shapriya, Coco Beach na Kwajionee
.
“Ni kweli ilikuwa twende kuzindua kwenye maeneo yenu lakini… lipo agizo ambalo lilitolewa na Serikali kuzuia mikutano katika mikoa hii, kupitia kwenu ipo haja ya kufungua mikutano ili demokrasia ipanuke zaidi,” alisema Nape na kuongeza:
“Amri hii kwa mtazamo wangu inabaka demokrasia, lazima mikutano iruhusiwe kama hali ni mbaya, kazi ya Serikali ni kulinda huo usalama… nitakwenda kushauriana nao ili mikutano ifunguliwe, sidhani kama masikio yanaweza kuzidi kichwa.”
Akizungumzia hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maisha Maganga alisema Serikali haijatengua agizo hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates