Social Icons

Alhamisi, 19 Juni 2014

Taylor hataki kufungwa jela Uingereza

Taylor alihukumiwa jela miaka 50 kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu


Taylor alifungwa jela kwa uhalifu dhidi ya binadamu na anakataa kutumikia kifungo hicho Uingereza akisema kuwa ananyimwa haki ya kufurahia maisha yake.

Mawakili wake wanasema kuwa kuzuiliwa kwake nchini Uingereza kunakiuka haki za binadamu kwa sababu ni mbali sana na yumbani kwa familia yake kuweza kusafiri huko kumuona.Charles Tayor anatumikia kifungo cha miaka hamsini jela kwa makosa ya ubakaji na kutumia watoto kama wanajeshi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone.

Wanasema kuwa badala ya kutumikia kifungo Uingereza, aruhusiwe kutumikia kifungo hicho nchini Rwanda, pamoja na wafungwa wengine waliohukumiwa na mahakama maalum ya umoja wa mataifa kuhusu Sierra Leone.
Pia wanasema anahofia kushambuliwa na wafungwa wengine katika gereza la Frankland, Kaskazini mwa Uingereza

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates