.
Serikali ya Uganda imekipiga marufuku kituo cha runinga cha NTV kufanya habari yoyote inayohusu ikulu au rais wa Uganda baada ya kuonesha picha ya rais Yoweri Kaguta Museveni akiwa amelala bungeni.
Meneja wa masuala ya vyombo vya habari wa serikali ya Uganda, Dennis Katungi aliiambia AFP sababu za kuifungia NTV kuonesha habari za ikul/rais.
“Wao wanafahamu kabisa kuwa rais huwa anatabia ya ku-meditate halafu bado wanaenda nje wanasema alikuwa amelala.” Alisema Katungi.
Nae msemaji wa serikali ya Uganda, Ofwono Opondo alithibitisha hatua iliyochukuliwa dhidi ya NTV Uganda ambayo ni sehemu ya National Media Group .
“Tumewasimisha kutotoa habari zote zinazomhusu rais kwa kuzingatia uhusiano wetu na wao.” Amesema Ofwono na kukituhumu kituo hicho kwa upungufu wa weledi na kuegemea upande mmoja.
Hata hivyo alisisitiza kuwa wamesimamishwa kwa muda na sio moja kwa moja.
Rais Museveni ana umri wa miaka 69 hivi sasa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni