Social Icons

Jumatatu, 30 Juni 2014

Giggs ;Sikuwa tayari kuwa mkufunzi

Giggs anasema kuwa uteuzi huo ulikuwa mapema kuliko alivyotarajia.

Giggs alichukua hatamu kama kaimu kocha mwisho wa msimu uliopita baada ya kocha David moyes Kutemwa kufuatia msururu wa matokeo duni tangu achukue hatamu Old Trafford.
Giggs aliyekuwa kocha katika mechi nne za mwisho alitwaa ushindi katika mechi 1 akashindwa moja na kisha akatoka sare katika mechi ya mwisho Manchester united ilipomaliza msimu katika nafasi ya 7 .

Giggs aliyasema hayo alipokuwa akikamilisha kozi ya ukufunzi akijitayarisha kusaidiana na Louis van Gaal Old Trafford .
Giggs alistaafu kama mchezaji msimu uliopita baada ya kuiwakilisha Man united katika mechi 963 na kufunga mabao 168

NAIBU KATIBU MKUU CUF BARA ANUSURIKA KATIKA AJALI


Naibu Katibu m kuu mpya wa CUF pia Mbunge wa viti Maalum Magdalena Sakaya akimshukuru Mungu baada ya kunusurika katika ajali na Lori kwenye makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere Dar

MAGAZETI LEO

 






LADY JAY DEE AWEKA HISTORIA HUKO KENYA.


Zilikuwa ni shangwe zakupitiliza pale mkali kutoka tzee Jaydee ilipofika zamu yake ya kupanda jukwaani, unaambiwa vile amepanda tu, uwanja mzima uliokuwa umefurika mashabiki, ulikuwa umeanza kupiga kelele zikisema yahayaa, ilikuwa ni kuanzia alipoanza kuimba nyimbo ya kwanza hadi ya saba, lakini watu wapi, walikuwa wamekazia na kuendelea kupaza sauti wakililia wimbo wa yahaya. 

Ni jambo ambalo hata lady Jaydee mwenyewe hakulitegemea.
Jaydee alifunguka nakusema “Tangu naanza kuimba wimbo wa kwanza mpk wa 7 watu wana scream tu, Yahaya, Yahaya. Duuuh! Kenya vipi?

Jumapili, 29 Juni 2014

Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal anatarajia shirikisho la soka duniani FIFA litawaruhusu wachezaji wake kunywa maji.


Fortaleza ni eneo linaloshuhudia viwango vya juu vya nyuzi joto.

Ni dhahiri kuwa mwili wa binadamu yeyote unastahili maji kwa hivyo hawa wachezaji naamini kuwa wanastahili kunywa maji ilikuzuia wasishikwe na kisunzi .Kocha huyo wa Manchester United ya Uingereza anasema kuwa utafiti uliofanywa kabla ya mashindano haya yanasema kuwa wachezaji wanapoteza maji lita nne ama zaidi kwa kila mechi wanayocheza katika jimbo hilo la Fortaleza.

Van Gaal kiwango cha joto ni juu mno
Van Gaal alitishia kuwapa wachezaji wake maji kwa wingi kando kando mwa uwanja iwapo FIFA haitahalalisha kuwepo kwa dakika moja au mbili ambapo mechi zitasimamishwa iliwachezaji wake wapige kopo la maji.
Kiungo wao Leroy Fer, ambaye anauguza jeraha la goti anasema kuwa Uholanzi ilipata kionjo tu cha kucheza katika hali ya kiwango cha juu mno cha joto baada ya kuwasili huko wakitoka Rio de Janeiro.
Fer anasema kuwa japo Uholanzi imezoea kucheza katika maeneo ya Uropa yenye baridi kali,Uholanzi itajikaza kisabuni kwani ni hali ileile itakayoikumba timu pinzani ya Mexico.

Sudan:Mwanamke mkristo bado yu taabani


Miriam Ibrahim na wanawe

Mawakili wa mwanamke mkristo nchini Sudan ,Meriam Ibrahim wamesema kuwa watawasilisha ombi mahakamani la kutaka mashtaka ya kughushi stakhabadhi bandia dhidi ya mteja wao kuondolewa.

Bi Ibrahim alikamatwa siku ya jumanne,siku ambayo mahakama ya rufaa ilibadilisha hukumu yake ya kifo hadi kuwa ya uasi.
Kufuatia uamuzi huo alijaribu kutoroka nchini humo kupitia stakhadhi za Sudan Kusini lakini akakamatwa katika uwanja wa ndege wa Khartoum.
Wakili mmoja amekiambia kitengo cha habari cha Ufaransa kwamba ana matumaini mamlaka itamuondolea mashtaka hayo na kumpatia paspoti ya Sudan ili kumruhusu kuelekea nchini Marekani.

HAKUNA CHA KUSEMA ZAIDI YA HONGERA HATA KAMA HATA CHUKUA TUZO ALIPOFIKA NI PAKUBWA.



Miguu ya Diamond Platnumz akiwa amesimama katika nyota yake iliyotengenezwa kwaajili ya msanii huyo kutoka Tanzania. Diamond anakuwa msanii wa kwanza kutoka nchini ambaye amepata mafanikio mpaka kupata 
nyota yake binafsi huko nchini Marekani. 

PICHA: DIAMOND, MAFIKIZOLO, DAVIDO,TIWA SAVAGE NA FALLY IPUPA KWENYE BET-PRE AWARDS VIP PARTY

DAVID
Diamond Platinumz anaiwakilisha Tanzania kwenye tuzo za BET zitakazofanyika huko Los Angeles, Marekani
.diaa 
Jana Diamond akiwa na wasanii wenzake wanaowania tuzo katika kipengele cha International Act (Africa) walihudhuria party ya utangulizi (BET Pre Awards VIP Party).
Fally Ipupa aliungana na wasanii wanaowania kipengele kimoja na Diamond ambao ni Davido, Mafikizolo na Tiwa Savage na Sarkodie (hayupo kwenye picha hizi).
ddavidoo diamondtiwa2Mafiki zoloTIWAFally Ipupa

MAGAZETI LEO







Dk Salim apongezwa


“Ni vizuri viongozi wakaandaliwa, isiwe mtu anaibuka tu anagawa hela halafu anashinda. Anatakiwa mtu atakayeweza kushughulikia matatizo ya Watanzania. Watanzania ni wapole na wavumilivu lakini wanazungumza. Hivyo anahitajika kiongozi atakayesikiliza mahitaji yao na kutoa suluhisho, si kutoa ahadi za uongo,” Dk Salim Ahmed Salim Kwa ufupi
  • Wakizungumza na gazeti hili wamesema, Dk Salim ametambua mchango alioutoa kwa taifa hivyo hana budi kuwaachia nafasi vijana nao wakatawala.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Waziri Mkuu mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim kusema kuwa hana mpango na hafikirii tena kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, wasomi na wanasiasa wamezungumzia kauli hiyo wakisema ni ya kishujaa inayofaa kuigwa na viongozi  wengine.Wakizungumza na gazeti hili wamesema, Dk Salim ametambua mchango alioutoa kwa taifa hivyo hana budi kuwaachia nafasi vijana nao wakatawala.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema Dk Salim hana anachotaka kukifanya kwani amelitumikia taifa kwa kipindi kirefu hivyo ameona ni busara kujiweka kando na kuwa mshauri.“Ni kauli nzuri na inayoheshimu busara, nafasi za uongozi alizofikia ni hakika zinatosha kulingana na umri wake na siasa chafu za nchini ni bora akawa pembeni na akatumika kama mshauri tu,” alisema Dk Bana.Naye mtaalamu wa masuala ya maendeleo na siasa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Idd Makombe  alisema Dk Salim amejifunza kutokana na  siasa za mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu zilivyochafuliwa.Alisema Dk Salim ameona bora ajiondoe kulinda heshima yake, kitendo kinachotakiwa kuigwa na wanasiasa wengine.“Mimi ninaamini kuwa kama Dk Salim angesimama katika uchaguzi uliopita au ujao na kusiwepo na siasa chafu, angeshinda bila ubishi,” alisema Dk Makombe.Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema kitendo cha Dk Salim kueleza kuwa ni lazima kuwa na sifa za ziada ndiyo ushinde, imedhihirisha jinsi CCM inavyowapata viongozi wake kwa njia zisizostahili.“Hata uwe na sifa za aina gani lakini lazima ufanye ujanja ujanja ndiyo ushinde. Sasa kwa watu ambao hawawezi kutumia mbinu hizo ndiyo kama Dk Salim, anaona bora akae kando kwani haziwezi mbinu hizo,” alisema Nyambabe.Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema, Dk Salim anatakiwa kuandika kitabu kuelezea yaliyojiri tangu awamu ya kwanza ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere hadi awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa katika mchakato wa kumpata mgombea urais.Alisema kutokana na kuwa na uzoefu wa kimataifa alimshauri Dk Salim atumie kitabu hicho kuelezea uzoefu wa mataifa mengine kuwapata wagombea urais unavyokuwa akifananisha na chama chake CCM ili kiwe ngazi na  tunu ya taifa kwa kizazi kijacho.

Jumamosi, 28 Juni 2014

UK yakumbwa na uhaba wa mbegu za kiume

Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.


Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana wasiwasi kwamba baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.

Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.
Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi walipendelea kuficha majina yao.
Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta watoto wao wenyewe.
Hatahivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiume bado upo.
Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya kigeni.
Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005.

Zungu asuruhisha mvutano wa Warema na Kafulila.

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu (kushoto) akijaribu kuwasuluhisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kulia) na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila katika Viwanja vya Bunge Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Dodoma. Vita kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila imeingia katika sura mpya baada ya mbunge huyo, kuwaeleza wapigakura wake kuwa endapo litatokea jambo lolote baya kwake, mhusika namba moja ni mwanasheria huyo.
Wakati Kafulila akisema hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi amemtaka mbunge huyo  kuonyesha uanaume wake kwa kuzungumza tuhuma zake akiwa nje ya Bunge.
Maswi aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye semina ya wizara hiyo na waandishi wa habari huku akisisitiza kwamba yeye ni msafi na yupo tayari kuchunguzwa na yeyote. “Nina usongo naye,” aliongeza Maswi.
“Mimi sichukui rushwa, sasa mtu anaokota vikaratasi vya kufungia vitumbua, anakwenda kutoa tuhuma zake…Alipomaliza kutoa tuhuma zake ndani ya Bunge nilimpigia simu nikamwambia kama yeye ni mwanaume, azungumze akiwa nje ya Bunge na siyo kutegemea kinga ya Bunge.
“Na akisema nje ya Bunge nampeleka mahakamani akathibitishe madai yake…Kwanza yuko mkononi, mwenzake (jina linahifadhiwa) hachangii tena hoja kwenye Wizara ya Nishati, nina tuhuma zake za kuhongwa,” alisema Maswi.
Maswi alikuwa akizungumzia tuhuma zilizoibuliwa bungeni na Kafulila akiwahusisha mawaziri wawili na Sh200 bilioni zilizochotwa kwenye akaunti ya Escrow, iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Tanesco na Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.
Akiomba mwongozo wa Spika bungeni jana, alisema wakati akichangia katika hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Spika Anne Makinda alielekeza kuwa apeleleke ushahidi wa ufisadi huo mezani kwake ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Alisema waliwasilisha ushahidi huo yeye na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika,  mezani kwa Spika lakini hadi leo hawajui aliupeleka wapi zaidi ya kuambiwa kwamba Waziri (hakumtaja) anautumia kukosoa.
“Mwenendo wa jambo hili tangu ulipoanza na wakati wa hotuba ya Waziri Mkuu na baadaye Wizara ya Nishati na Madini linaleta shaka kuhusu dhamira ya kiti kulishughulikia na limekuwa likihatarisha maisha yangu na wengine,” alisema.
 Alisema juzi akiwa bungeni Werema alionyesha kusudio la kutaka kumpiga na baadaye nje ya Bunge alitangaza kukitoa kichwa chake.
 “Nasimama hapa kuwaeleza wananchi wa jimbo langu, kitakapotokea kitu chochote kwangu muhusika wa kwanza atakuwa yeye kwasababu ya kauli hiyo ya kusema kuwa atachukua kichwa changu,” alisema.
Kafulila alitaka kufahamu Spika Makinda analitolea uamuzi gani ili kusudi liweze kufikia mwisho.
Akijibu Spika Makinda, alisema alimwandikia barua lakini kabla ya kuiona, akalisikia jambo hilo katika vyombo vya habari, “Hizo ni adabu hizo? Siyo adabu.”
Alisema suala hilo limeshatolewa uamuzi kamili kwasababu limeshapelekwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
“Ma-document (nyaraka  zako zote zinakwenda huko, ulitegemea sisi tufanye hukumu hapa? Ndivyo tunavyofanya? Hata ulipoleta (suala hilo) juzi mimi nilikushangaa sana,” alisema.
Alisema Kafulia wapo naye katika Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)  na kumsifia kuwa ni mmoja wa vijana hodari lakini kwa jambo hilo ameona (Spika) hajalishughulikia vyema.
“Sasa tunaanza kupata mashaka ni suala la kawaida ama siyo la kawaida? Nataka kukwambia kuwa suala hili liko kwa CAG na Takukuru sasa hivi,” alisema na kumtaka kuendelea kupeleka nyaraka za ushahidi hukohuko.
Kuhusu usalama, Makinda alisema: “Wewe umemchokoza na yeye akachokozeka, mnapotumia lugha mbaya mjue kuwa kila mtu ni binadamu. Tulieni suala la IPTL  lina utaratibu wake.”
 Alisema hakuna namna nyingine zaidi ya kupeleka nyaraka hizo kwa CAG na Takukuru.
“Sasa mnakaa mnatusambazia makaratasi haya sisi tufanye nini. Jambo ambalo mtu anajua lina tatizo anakuwa na utulivu. Kama unajiamini unakuwa na utulivu. Kama hujiamini unakuwa hauna utulivu,” alisema.
Alipoulizwa kuhusu kauli ya Maswi, Kafulila alisema ameshazungumza jambo hilo nje ya bunge na kwamba hana hofu yoyote kwa kuwa anauhakika taarifa anazozisema ni sahihi.
Kuhusu yeye kutumiwa na Mbunge wa Musoma Vijijini kuwatuhumu Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake Maswi, alisema hakuna jambo hilo siyo la kweli.
“Juzi tulikutana na waandishi na nilitaka akaunti ya Kampuni ya Uwakili ya Mkono (Mkono & Co. Advocates) ichunguzwe. Itakuwaje mtu huyo huyo anipe documents (nyaraka)?” alihoji Kafulila.

Alisema kinafanyika sasa ni dalili zinazoonyesha kuwa viongozi hao wameanza kutapataka kwa kuwa wanafahamu malipo hayo hayakufanywa kwa njia halali.
“Huko ni kutapatapa hoja hapa ni Sh200 bilioni zilizochukuliwa. Naamini watachukuliwa hatua,” aliongeza.
Katika tuhuma zake Kafulila, alimuunganisha pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine, wakiwamo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na  Serikali, wote akiwataja tu kwa vyeo bila majina.
Mawaziri waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).  Ingawa Kafulila hakutaja kwa majina, Waziri wa Nishati ni Profesa Sospeter Muhongo, wa Fedha ni Saada Mkuya, Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Nishati) ni Eliakim Maswi na AG ni Frederick Werema.
Kafulila alitoa tuhuma hizo bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2014/1

EVANS AVEVA AMALIZA KAMPENI ZA URAIS SIMBA KWA KISHINDO

 Mgombea wa nafasi ya urais Evans Aveva, akiwa na Mlinzi wake 'Board Guard' (nyuma) akijinadi kwa wanachama, wakati wa mkutano wake wa kampeni za mwisho na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu wa Klabu hiyo kesho, kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuiongoza Klabu ya Simba kwa kipindi kijacho cha miaka minne. Hitimisho hilo la kampeni zake limefanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali, akimnadi mgombea Urais Evans Aveva.
 Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
 Baadhi ya wanachama wa Simba waliohudhuria mkutano huo.
 Baadhi ya wazee wa Simba waliohudhuria mkutano huo....
 Meza kuu.

*Amwaga sera kabambe, kula sahani moja na mafisadi, makomandoo

Na Majuto Omary
WAKATI Kampeni za uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba zikifungwa rasmi leo kuelekea zoezi kamili la uchaguzi huo linalotarajia kufanyika kesho (Jumapili) kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, mgombea anayepigiwa ‘chapuo’ kubwa na wanachama wa klabu hiyo katika nafasi ya Urais, Evans Aveva amemaliza kampeni zake kwa kishindo na kutoa ahadi ya kula sambamba na Makomandoo na mafisadi wanaoihujumu klabu hiyo.

Mbali ya ahadi hiyo, Aveva pia amesema, iwapo atapewa ridhaa ya kuiongoza Simba, atarudisha heshima ya klabu hiyo kwa kutwaa ubingwa na kushiriki mashindano ya kimataifa kwa kusajili wachezaji bora wazawa wenye uwezo na kuongeza wageni iwapo watahitajika baada ya kukosa mzawa wa kumudu nafasi husika. 
Akizungumza katika mkutano wake wa mwisho uliofanyika kwenye hotel ya Hyatt Regency Kulimanjaro, Aveva alisema kuwa atatumia vyombo vya sheria kupambana na wauzaji bidhaa za klabu hiyo wanaotumia nembo ya Simba ili kukusanya mapato ya klabu kwa ajili ya kutumika katika maendeleo ya klabu.

Aidha, Aveva alisema kuwa katika kuhakikisha anaondoa mianya hiyo, atatumia matawi ili kukamata bidhaa hizo na lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuweka utaratibu ambao utaiwezesha klabu hiyo kujikusanyia mapato na kuweza kujitegemea.
“Bidhaa zenye nembo ya klabu zinauzwa kiholela na kufaidisha wachache huku klabu ikiendelea kuwa tegemezi, mimi sitavumilia hali hiyo na nitahakikisha nakula nao sahani moja ili kuokoa klabu,” alisema Aveva.
Alisema kuwa uongozi wake utakuwa wa kushirikisha zaidi Matawi na ataunda kamati mbali mbali ili kuweza kufanikisha mpango mkakati wake wa kuendeleza klabu.
“Sitaweza kufanya kila kitu mimi, nitaunda kamati ambazo zitawajibika katika kamati ya utendaji na kufanya majukumu hayo, lengo kubwa ni kufikia lengo na kuhodhi madaraka, nitafanya hivyo kwa maendeleo ya klabu na wala si vinginevyo,” alisema.

Pia alisema kuwa atasajili wachezaji ambao wataiwezesha timu hiyo kufanya vyema katika ligi na kurejesha hadhi na heshima yake ya kushiriki mashindano ya kimataifa.
Uchaguzi huo utashirikisha jumla ya wagombea 27 ambapo mbali na Aveva, nafasi hiyo pia inagombewa na Andrew Tupa. Wagombea  wengine ni Swedi Mkwabi, Bundala Kabulwa , Geofrey Nyange na  Jamhuri Kihwelo ambao wanagombea nafasi ya makamu Rais.

Wanaowania ujumbe ni Said Tulliy,  Yasini Mwete, Ally Suru,  Rodney Chiduo,  Said Pamba,  Ally Chaurembo , Abdulhamid Mshangama , Chano Almasi,  Damian Manembe,  Ibrahim Masoud, Kajuna Noor,  Hamisi Mkoma,  Alfred Elia na Saidi Kubenea.
Wagombea wengine ni Idd Mkamballah, Juma Mussa, Maulid Abdallah na Collin Frisch.Wagombea kwa upande wa wanawake ni Asha Muhaji, Amina Poyo na Jasmine Badour

Ijumaa, 27 Juni 2014

Mdhamini wa Luis Suarez ajiondoa

Mchezaji wa Italy Chiellini na Luis Suarez
Kampuni ya kamari ya mtandaoni 888 poker imesema ''imeamua kusitisha mkataba wake na mchezaji huo mara moja''.

Walitaka aondolewe katika michuano ya kombe la dunia.Na kweli walifanikiwa.''Kila mtu anajua ni nini kilichomfanya Luis.

''Walimuondoa katika mechi hizo kama mbwa'' alisema Lila Piris Da Rosa bibiye Suarez.

''Mchezaji huyo wa miaka 27 anayeichezea kilabu ya Liverpool alipigwa marufuku ya miezi minne na shirikisho la soka duniani FIFA baada ya kupatikana na hatia ya kumng'ata Chiellini katika mechi ya kombe la dunia.
"
Suarez hawezi kuchezea kilabu yoyote ama taifa lake hadi mwisho wa mwezi Oktoba.

Atakosa kushiriki katika mechi zilizosalia katika kombe la dunia nchini Brazil.
Uruguay itacheza na Colombia katika mechi za kumi na sita bora siku ya jumamosi baada ya kufuzu katika kundi la 'Da' nyuma ya Costa Rica.
Suarez alijiunga na kampuni ya 888poker kama mjumbe wake duniani siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia na kutoa baadhi ya kanda za video za shajara ya mtandao wake ikiwemo moja ya bao lake wakati wa ushindi wa taifa lake dhidi ya Uingereza.

Ukraine,Georgia na Moldova watia sahihi


Rais Petro poroshenko katikati baada ya kutia sahih mkataba wa ushirikiano na ulaya.

Makubaliano hayo ambayo yatayaunganisha pamoja mataifa hayo na kuyaegemeza Magharibi kiuchumi na kisiasa, haswa ndio msingi wa mgogoro ulioko Ukraine.

Usitishaji wa vita kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaounga mkono Urusi, mashariki mwa Ukraine, unakamilika Ijumaa hii.Urusi imesema kuwa hata ingawa kutia saini mkataba huo ni haki ya taifa lolote, kunaweza kuleta madhara mabaya baadaye.

Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko aliusifu mkataba huo akisema ni siku ya kihistoria katika taifa la Ukraine baada ya siku ya Uhuru wa taifa hilo mwaka 1991.
Ameutaja kuwa dalili ya imani na nia isiyoweza kuvunjwa.
.
Poroshenko pia amesema kuwa ameuona mkataba huo kama mwanzo wa mchakato wa kujiunga na Umoja wa bara Uropa,''Ukraine inadhibitisha chaguo lake la kitaifa, kujiunga na EU" alisema.
Kwengineko, rais wa Umoja wa bara Uropa, Herman va Rompuy ametaja kuwa "siku kuu kwa bara Uropa".
''Umoja wa bara Uropa unasimama pamoja nanyi, leo zaidi ya siku nyingine yoyote awali" aliwaambia viongozi wa nchi hizo tatu, akiongeza kuwa hakuna chochote katika mikataba hiyo ya makubaliano kitakachoiletea madhara Urusi kwa njia yoyote ile.
Naibu waziri wa maswala ya nje wa Urusi, Grigory Karasin ''ameliambia shirika la habari la Interfax kuwa hatua hiyo huenda ikazua madhara.
Kutiwa sahihi kwa mkataba huu muhimu, kwa hakika ni haki ya taifa lolote lile" alisema.
Ila tu matokeo ya Ukraine na Moldova kutia saini mkataba huu bila shaka yatakuwa mabaya".
Mapema, mshauri mkuu wa Kremlin, Sergei Glazyev alimtaja Poroshenko kuwa mwanachama wa Nazi na kuwa uchaguzi wake kuwa rais haukuwa wa haki kwani sehemu kubwa ya Ukraine haikupiga kura katika uchaguzi wa mwezi Mei.
Alizidi kusema kuwa Poroshenko hana haki kikatiba kutia sahihi mkataba huo, jambo ambalo litadhuru uchumi wa Ukraine.

Mnyika:Waasi Chadema wamehongwa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema watu wanaojiita wanachama wa chama hicho wakiendesha uasi, wanapewa fedha na chama kimoja kikubwa nchini ambacho hakimo ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).


Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika, katika mkutano na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, madai yaå kundi la watu waliojiita kuwa ni wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho hayana ukweli wowote na kuwa watu hao wanatumika kisiasa.

“Tunawajua na tunaelewa njama na mipango yao yote, lakini kwa leo siwezi kuwataja kwa sababu nikiwataja ndio mtakaowafanya habari kubwa na wenyewe watarudi kutushambulia kuwa hatukujibu hoja, lakini katika muda mwafaka ipo siku tutawataja hivyo kwa leo ngoja niishie kujibu hoja za msingi,” alisema Mnyika.

Alisema viongozi na chama hakijavunja katiba yake kwa kujiunga kushirikiana na vyama vingine vya siasa kuanzisha Ukawa.

Aidha, Mnyika alisema kuwa tuhuma zilizotolewa na watu hao kuhusu ubadhirifu wa fedha ndani ya Chadema siyo za kweli kwa kuwa hesabu za fedha za Chadema zimekwisha kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na taarifa yake kupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Akizungumzia tuhuma kuwa viongozi wa Chadema wanavunja katiba kwa kujiunga na Ukawa, Mnyika alisema kuwa Ukawa siyo chama cha siasa bali ni umoja wenye lengo la kuleta mshikamano mzuri na vyama vingine na kwamba katiba ya Chadema inaruhusu chama hicho kuwa na uhusiano mzuri na vyama vingine vya siasa.

“Chama hiki kinaongozwa na katiba na kwa kweli hakuna kifungu chochote kwenye katiba kilichovunjwa kwenye uamuzi wa chama kuanzisha ushirikiano na vyama vingine vya siasa na makundi mbalimbali katika kile kinachoitwa Umoja wa Katiba ya wananchi yaani Ukawa,” alisema Mnyika.

Alisema kuwa katiba ya Chadema imeaninisha utaratibu wa chama kushirikiana na vyama vingine katika nyanja tatu ambazo ni ushirikiano wa kuunganisha vyama ili kuwa na chama kimoja cha siasa, ushirikiano wa kufanya miradi ya pamoja na ushirikiano wa kushirikiana katika shuguli za kisiasa.

Alisema kuwa Ukawa siyo chama cha siasa hivyo kwa kujiunga na Umoja huo Chadema haijavunja katiba yake, bali wanaosema kuwa imekosea kwa mujibu wa katiba yake kujiunga na Ukawa ni kwa sababu tu hawaijui katiba ya chama hicho.

Mnyika alisema kuwa ushirikiano kwenye uchaguzi ambao watu hao wameurejea kwenye mazungumzo yao kwa kutamka kwamba Chadema inakusudia kushirikiana na vyama vingine kwenda kusimamisha mgombea mmoja, wakisema kuwa ni ukikwaji wa katiba pia siyo sahihi.

Alisema kuwa chama kinayo haki ya kikatiba ya kushirikiana na vyama vingine kwa kuweka mipango mbalimbali ya kimaendeleo ikiwamo ushirikiano wakati wa uchaguzi.

Alisema kuwa uamuzi wa chama kuacha kuteua mgombea kupisha chama kingine au chama kuachiwa na chama kingine unakamilika wakati wa uchaguzi na kuwa kabla ya hapo ni maamuzi ya matazamio na mipango tu.

Alisema kuwa jambo hilo siyo geni kwani mwaka 2007 Chadema ilisaini tamko la ushirikiano wa vyama vya siasa vya CUF, TLP, Chadema na NCCR na kuwa kama wanaopinga uamuzi huo wangekuwa ni wanachama hai wa Chadema, wangepinga tangu wakati huo.

Akizungumzia suala la ubadhirifu wa fedha ambalo limeibuliwa na watu hao waliojiita wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema, Mnyika alisema kuwa madai yao hayana ukweli wowote kwa kuwa hesabu zote za fedha za Chadema tayari zimekwishakaguliwa na CAG na taarifa yake kupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Mnyika alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutoa taarifa za fedha za vyama vyote vya siasa ambavyo tayari vimekwishakaguliwa ili ukweli juu ya suala hilo pia ujulikane kwa umma wa Watanzania.

“Mimi kama msemaji wa Chadema nitoe wito kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, kuweka wazi ripoti za vyama vyote vya siasa alivyovikaguka kwa umma ili ukweli ujulikane,” alisema Mnyika.

Mnyika alisema kuwa Chadema kama taasisi siyo chama cha ufisadi na ubadhirifu na kuwa chama hicho hakiwezi kuvumilia ufisadi wa aina yoyote wa ndani au wa nje ya chama na kwamba chama hicho ndicho kilichotaka sheria ibadilishwe ili CAG aanze kukagua hesabu za vyama vya siasa.

NJAMA ZA HUJUMA
Baada ya kujibu hoja hizo, Mnyika aliwageukia watu walioanzisha madai hayo akisema kuwa wengi wao siyo wanachama wa Chadema, baadhi yao ni wale ambao tayari walishafukuzwa uanachama na wachache ambao ni wanachama halali wa Chadema aliwaita kuwa ni wasaliti.

Alisema kuwa licha ya watu hao kudai kwamba wako 82, lakini waliojiorodhesha kwenye nyaraka alizozipata ni watu 32 pekee na baada ya kuchunguza majina hayo imebainika kuwa zaidi ya watu 10 wamegushiwa saini zao.

Mnyika alisema kuwa uchunguzi uliofanywa na umebaini kuwa watu hao wametumwa na kufadhiliwa na chama kimoja cha upinzani ambacho hakimo kwenye Ukawa kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa juu serikalini.

Alisema kuwa chama hicho pamoja na viongozi wa Serikali waliojihusisha na mpango huo wa kukichafua Chadema wanawafahamu kwa majina pamoja na kiasi cha fedha walichopewa kuwezesha mpango huo.

BARAZA KUU KUKUTANA JULAI
Mbali na kujibu hoja hizo, Mnyika alisema kuwa kati ya Julai 18, mwaka huu chama hicho kitafanya mkutano wake wa Baraza Kuu Taifa kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya chama hicho.

Aidha alisema kuwa chama hicho kinaendelea na uchaguzi wake wa ndani katika ngazi mbalimbali na kwamba kabla ya kuadhimisha siku ya mafisadi, Septemba 15, mwaka huu watakuwa wamekamilisha uchaguzi wa ndani hadi ngazi ya taifa.

ANGALIA PICHA MBINU MPYA YA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA YABAINIKA MKOANI KILIMANJARO

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,SACP,Robert Boaz akitoa dawa za kulevya katika mikoba ya kike ambayo imekamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,SACP,Robert Boaz akiwaonesha waandishi wa habari(hawako pichani)moja ya mikoba iliyotumika kufichia dawa za kulevya kwa ustadi mkubwa.
Dawa za Kulevya ambazo hazijafahamika ni aina gani zikiwa katika mifuko maalumu.
 
 
Blogger Templates