Social Icons

Jumatano, 20 Novemba 2013

WAPOTEZA MAISHA,50 WAKIFUKIWA NA KIFUSI BAADA YA JENGO KUPOROMOKA AFRIKA KUSINI


Taswira za jengo lililoporomoka eneo la Tongaat Kaskazini mwa mji wa Durban nchini Afrika Kusini na kuua watu wawili mpaka sasa. (PICHA: eNCA)
Watu wawili wamepoteza maisha na wengine takribani 50 wakifukiwa kwenye vifusi baada ya paa la jengo la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka eneo la Tongaat Kaskazini mwa mji wa Durban nchini Afrika Kusini.
Watu 29 wameweza kuokolewa kutoka katika jengo hilo.
Madaktari kutoka kampuni ya Netcare 911 walifika kutoa huduma ya kwanza katika eneo hilo la Tongaat.
“Shughuli hii itachukua muda mrefu. Itatuchukua muda kuwafikia wale waliokwama,” alisema msemaji wa kampuni hiyo.
Hata hivyo ni mapema mno kujua sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates