Dk Sengondo Mvungi.PICHA|MAKTABA
Hospitali
ya Millpark ya Johannesburg, Afrika Kusini, imesema madaktari
waliokuwa wakimtibu aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Dk Sengondo Mvungi walibaini kuharibika kwa ubongo wake kutokana na
kumwagika kwa maji yanayoutunza ambayo kitaalamu yanaitwa
‘cerebrospinal fluids’ au CCF.
Msemaji
wa Hospitali hiyo, Tebogo Nyembezi alisema Dk Mvungi alicheleweshewa
tiba baada ya kupata tatizo la maji hayo yanayotunza ubongo kumwagika
mara baada ya kujeruhiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni