Katika
hali ya kuonyesha kwamba wafanyabiashara wa eneo la kariakoo hawataki
wala kusikia kuhusu mashine za T.R.A,Wafanyabiashara hao wameamua
kufunga mabango katikati ya mitaa yakiwa na ujumbe wa kupinga matumizi
ya mashine hizo,ONAVIEWS.BLOG ilipita mitaa mbali mbali Kongo,Mchikichi,Swahili,Kipata,Uhuru na mingine.
Leo
ni siku ya pili kwa wafanyabiashara hao kugoma kufanya biashara,Swali
la msingi je Serikali inaonaje hali hii ya wanainchi kukosa huduma?na
pia huu ni mkoa wa nne sasa baada ya Mbeya,Morogoro na Mtwara.picha zote na 0naviews.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni