Social Icons

Jumanne, 19 Novemba 2013

RONALDO APIGA HAT TRICK URENO NA UFARANSA ZAFUZU KOMBE LA DUNIA

                                                                   BENZEMA
Ufaransa imefanikiwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia baada ya kuigeuzia kibao Ukraine na kuichapa mabao 3-0.

Awali Ukraine ilishinda kwa mabao 2-0 ikiwa nyumbani na kuweka matumaini ya juu kusonga mbele katika mechi hiyo ya marudiano ugenini.

Lakini leo kwa mabao ya Mamadou Sakho aliyefunga mawili na Karim Benzema, Ufaransa imetinga fainali ya Kombe la Dunia.

Ilionekana ni vigumu kwa Wafaransa kusonga mbele baada ya kufungwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza.
 





Mabao matatu yaliyopigwa na Cristiano Ronaldo yameivusha Ureno kucheza Kombe la Dunia mwakani.

Ushindi huo wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji Sweden ambao nao mabao yao mawili yalifungwa na nahodha, Zlatan Ibrahimovic.

Katika mechi ya kwanza, Sweden ikiwa ugenini ilikutana na kipigo cha bao 1-0.

Ureno ilianza kupata bao kupitia Ronaldo, wenyeji Sweden wakasawazisha na kufunga mabao mawili kupitia Ibrahimovic.

Lakini Ronaldo alipiga mabao mawili harakaharaka na kumaliza kabisa matumaini ya wenyeji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates