Usiku
wa kuamkia leo nguzo za umeme zaidi ya tano zimeanguka baada ya nguzo
moja kugongwa na gari na kisha kuziangusha zingine na kusababisha moto
na kishindo kikubwa kilichowashitua wakazi wa maeneo ya Bamaga Mwenge.
Tukio hilo lingeweza kuleta madhara makubwa iwapo lingetokea wakati
kuna foleni ya magari kama inavyokuwa nyakati za asubuhi na jioni katika
barabara hiyo ya Ali Hassan Mwinyi, jirani na maeneo ya Chuo Cha Posta,
TBC1 na TSN Super Market na kituo chake cha mafuta.
Hivi sasa barabara ya Shekilango kutokea Ali Hassan Mwinyi haipitiki.
Magari yaliyosababisha kadhia hii, gari ndogo na Lori la mchanga,
yalikamatwa usiku lakini madereva wake walitoroka. Picha zote ni za
tukio hilo kama zinavyonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni