Social Icons

Jumatano, 20 Novemba 2013

HUYU NDIO KOCHA MPYA WA SIMBA NI LOGARUSIC WA CROATIA


Zdravko Logarusic raia wa Croatia.
Baada ya kuwatimua makocha wake, Abdallah Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’, Simba sasa imemchukua kocha Zdravko Logarusic raia wa Croatia.
Tayari Simba imemaliza mazungumza na kocha huyo na anatarajia kutua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kusaini mkataba na mara moja kuanza kazi.Kabla ya hapo, Logarusic alikuwa kocha wa Gor Mahia ya Kenya aliyoifundisha kwa misimu miwili akisha nafasi ya pili.Msimu huu ulikuwa wa mwisho, lakini aliondoka katikati na nafasi yake kuchukuliwa na Bobby Williamson ambaye kuna gazeti liliandika anajiunga na Simba, kitu ambacho hakikuwa sahihi.Baadaye Bobby alikanusha kuwa amefanya mazungumzo na Simba na ataendelea kubaki Kenya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates