KLABU ya
Newcastle imeanza mazungumzo ya kumchukua winga wa Manchester United,
Wilfried Zaha kwa mkopo ifikapo Januari. Wawakilishi wa mchezaji huyo wa
England walikutana na viongozi wiki iliyopita kujadili uwezekano wa
mkopo wa miezi sita, na kocha wa United, David Moyes ametoa wazo la
kumpatia Zaha timu atakayokuwa akipata naba kikosi cha kwanza katika
Ligi Kuu.
Zaha,
mwenye umri wa miaka 20, alikuwa mchezaji wa mwisho kusajiliwa na Sir
Alex Ferguson kabla hajastaafu, lakini amecheza mechi moja tu ya Kombe
la Ligi, maarufu kama Capital One chini ya Moyes.
Katika mazungumzo: Wilfried Zaha yupo katika mazungumzo na Newcastle United juu ya uwezekano wa kwenda kucheza kwa mkopo
Mchezaji
huyo wa zamani wa Crystal Palace aliichezea mechi ya kwanza England
dhidi ya Sweden mwaka jana, lakini kutokana na kukosa nafasi katika
klabu yake, amejikuta akirejeshwa kikosi cha vijana chini ya umri wa
miaka 21. Zaha amekataa kurejea Palace.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni