Social Icons

Jumatatu, 25 Novemba 2013

Mh. Lowassa aongoza harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar


 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiburudika kwa kucheza muziki sambamba na wakina Mama wakazi wa Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam,Mwishoni mwa wiki wakati alipokwenda kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo.Zaidi ya Sh. Mil. 100 ziliweza kupatikana kwenye harambee hiyo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipena mikono na Wakazi mbali mbali wa Kata ya Saranga,Kimara wakati akiendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisisitija jambo kwa wananchi wakazi wa Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
 Diwani wa Kata ya Saranga (CHADEMA),Mh. Ephraim Kinyafu akizungumza machache wakati wa harambee hilo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa NEC (CCM) Wilaya ya Kinondoni,Kalist Lyimo akisisiza jambo kwa wakazi wa Saranga,Juu ya umuhimu wa kuchangia harambee hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates