Cameroon imefanikiwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia baada
ya kuichapa Tunisia kwa mabao 4-1.
Mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare bila kufungana na
jana Cameroon wakaonekana wako safi zaidi wakiwa nyumbani.
Mabao yalifungwa na Pierre Webo, Moukadjo na mkongwe Jean
Makoun akafunga mawili.
Cameroon imekuwa timu ya tatu ya Afrika kujihakikishia
kufuzu baada ya Ivory Coast na Nigeria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni