Social Icons

Jumatano, 31 Desemba 2014

DIAMOND NA ZARII ZE BOSS NI NOMA EMBU JIONEE MWENYEWE.







Rais Jammeh:'Bado niko mamlakani'

Rais wa Gambia Yahya Jammeh
Rais wa Gambia amesema kuwa bado analiongoza taifa hilo la Afrika magharibi baada ya vikosi vyake vya usalama kutibua jaribio la mapinduzi.
Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.
Hatahivyo hajulikani aliko.Milio mikali ya riasi ilizuka karibu na makao ya rais katika mji mkuu.
Bwana Jammeh alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mwaka 1994 na wapinzani wake wamekuwa wakimkosoa kwa uongozi wake wa kiimla.
Duru za kidiplomasia na zile za kijeshi zinasema kuwa wanajeshi kutoka kwa jeshi la ulinzi wa rais wanadaiwa kufanya shambulizi hilo katika makao ya rais mjini Banjul mapema siku ya jummane.
Serikali imekana kwamba kulikuwa na jaribio la mapinduzi katika taarifa iliotangazwa katika radio ya taifa.
Hatahivyo,bwana Jammeh baadaye alikiri kuhusu shambulizi hilo na kusema kuwa wanajeshi waaminifu wa Lamin Sanneh aliyemtaja kama mwenye aibu walivamia mji mkuu wa Gambia kutoka Senegal katika jaribio la kutaka kuipindua serikali yake.
Amesema kuwa wavamizi hao hatahivyo walikabiliwa na vikosi vya usalama na kuwaua wanne kati yao huku wengine wanne zaidi wakikamatwa.

WATU WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUTOROKA NA ALBINO MKOANI MWANZA


 

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu wanne akiwemo baba mzazi wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Albinism aliyetekwa nyara na watu wasiojulikana usiku wakiwa wamelala na kuondoka naye kusikojulikana hali iliyozua hofu kubwa kwa jamii.

Amebainisha hayo kamishina msaidizi mwandamizi ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Bw.Valentino Mulowola wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amemtaja mtoto wa kike aliyetekwa nyara mwenye umri wa miaka minne Pendo Emmanuel mkazi wa kijiji cha Ndambi kata ya fukalo tarafa ya mwamashimba wilayani kwimba ambaye ni mlemavu wa ngozi amesema kuwa tarehe 27 Desemba mwaka huu majira ya saa nne na dakika 30 za usiku watu wasiojulikana walivamia nyumba ya Bw.Emmanuel Shilinde kwa kupiga jiwe mlango na kuvamia kisha wakamchukua mtoto mmoja kati ya watoto watatu waliokuwemo ndani ya nyumba hiyo kisha wakatoweka naye kusiko julikana.

Kufuatia hali hiyo makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania imetuma timu ya askali upelelezi watakao shirikiana na askari polisi mkoa wa Mwanza kuwasaka wahalifu walio husika kumteka nyara mtoto na kutoweka naye pasipojulikana pamoja na kutoa ahadi ya zawadi ya fedha kiasi cha shilingi milioni tatu kwa yeyote atakaye fanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao ambapo kikosi hicho kwa pamoja kimewatia mbaloni wahamiaji haramu saba raia wa Ethiopia na watanzania wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kusaidia wahamiaji haramu hao kuingia nchini kinyume cha sheria za nchi. 

MACHOZI YAWATOKA DIAMOND NA ZARI BAADA YA KUONA MABAKI YA MIILI KATIKA VITA YA KIMBALI NCHINI RWANDA





MTUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA APIGWA RISASI KATIKA HARAKATI ZA KUTAKA KUTOROKA MAHAKAMANI

Mtuhumiwa wa madawa ya kulevya raia wa Sierra Leone akiwa amepigwa risasi baada ya kutaka kuwatoroka askari magereza katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.












Jumatatu, 29 Desemba 2014

ALIYE KUWA WAZIRI WA KILIMO,MANSOUR HIMID AJIUNGA RASMI CUF,ZANZIBAR


Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akimpongeza Mhe. Mansour Yussuf Himid baada ya kuamua kujiunga na chama hicho na kumkabidhi rasmi kadi ya CUF katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.
Mwanachama mpya wa CUF Mansour Yussuf Himid akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, baada ya kujiunga na chama hicho katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.
Mwanachama mpya wa CUF Mansour Yussuf Himid akizungumza na wanachama wenzake , baada ya kujiunga na chama hicho katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.
Wanachama wa CUF wakionyesha kuunga mkono uamuzi wa Mansour Yussuf Himid kujiunga rasmi na chama hicho kwenye viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja. 

Aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mansour Yussuf Himid, amejiunga rasmi na chama cha wananchi CUF. Mhe. Mansour ambaye amewahi kuitumikia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushika nyadhifa mbali mbali ikiwemo ya Waziri wa Kilimo, amechukua uamuzi huo kwenye mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.

Baada ya kukabidhiwa kadi ya CUF na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, Mhe. Mansour amesema ameamua kujiunga na CUF baada ya kubaini na kuridhika kuwa chama hicho kimebeba matumaini mapya ya wazanzibari. Mhe. Mansour ambaye tayari alishateuliwa na chama hicho kuwa mshauri wa mikakati wa Katibu Mkuu wa CUF, amechukua kadi hiyo akiwa miongoni mwa wanachama wapya 108 waliojiunga na CUF kwenye mkutano huo.

Mapema akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amempongeza Mhe. Mansour kwa kuamua kujiunga na chama hicho hadharani, na kukiita kitendo hicho kuwa ni cha kijasiri. Akizungumzia mafanikio ya chama hicho, Maalim Seif amesema kimepata mafanikio makubwa katika mwaka unaomalizika wa 2014, na kutangaza maazimia mapya ya chama hicho kwa mwaka 2015.

Ametaja mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja na kuendelea kukubalika kwa chama hicho katika pembe zote za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Kuhusu maazimio ya Chama hicho kwa mwaka 2015, Maalim Seif amesema kimejipanga kuhakikisha kuwa kinashinda kwa asilimia kubwa katika uchaguzi mkuu ujao na kuweza kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa.

Hata hivyo amewataka wanachama wasibetweke kutokana na mafanikio yaliyopatikana, bali waongeze nguvu kuhakikisha kuwa malengo ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao yanafikiwa.

Ameongeza kuwa CUF pia kimejipanga kuimarisha uchumi na kujenga Zanzibar mpya itakayokuwa ya matumaini kwa Wazanzibari wote.

Katika hatua nyengine, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema katika uchaguzi mkuu ujao hatowazuia vijana kutetea haki yao iwapo watadhulumiwa.

“Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 nilifanya kazi kubwa ya kuwazuia vijana wasifanye vurugu pale hoteli ya Bwawani. Mwanzo niliwatuma wasaidizi wangu waende kuwaondosha lakini hakuna aliyesikia hadi nilipokwenda mwenyewe, tena waliondoka kwa shingo upande kabisa. Kwa hivyo uchaguzi mkuu ujao sina namna yoyote ya kuwazuia vijana kutetea haki yao”, alifafanua Maalim Seif.

Kabla ya mkutano huo Maalim Seif alifanya ziara ya kukagua uhai wa chama hicho katika vijiji vya Michamvi, Bwejuu, Jambiani na Paje ambako aliweka mawe ya msingi kwenye matawi ya chama hicho, pamoja na kupandisha bendera kwenye barza ya DAY OUT ya Paje.

NYALANDU ATANGAZA RASMI KUWANIA URAIS 2015


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo .
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
 Mwimbaji wa muziki wa Injili, Frola Nkone akiimba kutumbuiza wakati wa mkutano huo
 Mwanamuziki wa muizki wa Injili, Rose Mhando akiimba kutumbuiza wananchi katika mkutano huo wa Nyalandu
 Wasanii wa kikundi cha Makomandoo cha mjini Singida wakitumuiza wakati wa mkutano huo
 Wadau wakifurahia burudani wakati wa mkutano huo wa Nyalandu

 Steve Nyerere ambaye ni Msanii na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM, akizungumza kabla ya kumwaga vimbwanga vyake vya kuingiza sauti za viongozi mbalimbali wakati wa mkutano huo wa Nyalandu.

KABLA YA MKUTANO

 Nyalandu na Mkewe Faraja Kota wakiingia kwenye Kanisa la KKKT  Usharika wa Ilongelo kwa ajili ya ibada maalum. Pamona nao ni watoto wao Sera na Christopher kabla ya kwenda Uwanjani kutangaza azma yake ya kuwania Urais 2015
 Nyalandu na Faraja Kota wakiwa na watoto wao Sera na Christopher katika kanisa hilo 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro  Nyalandu akitoa neno la shukrani baada ya ibada maalum katika katisa la KKKT Usharika wa Ilongelo jimboni humo leo.
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili lkatika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akizungumza na viongozi wa shule ya Kiislam ambayo huhudumia watoto wa dini zote katika kata ya Ilongelo, shule hiyo ina watoto 74.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akisalimia waumini kwenye Kanisa la FPCT  katika jimbo la Ilongelo alipofika kwa ajili ya ibada maalum
 Waumini wakiwa katika kanisa la FPCT wakati wa ibada maalum aliyohudhuria Nyalandu leo
Nyalandu na Mkewe wakitoka katika Kanisa la FPCT baada ya kuhudhuria ibada maalum leo asubuhi. Na Bashir Nkoromo, Singida

Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.
Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.
Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.
Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.
"Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema Nyalandu
Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM", alisema.
Mkutano huo wa jimbo ambao ulipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo za wasanii wakiwemo kina Rose Mhando, ulifurika maelfu ya wananchi waliohamasika kumsikiliza Nyalandu.

UTAMU WA DAR KUELEKEA MWAKA MPYA (MVUA)





Alhamisi, 25 Desemba 2014

MERRY X-MASS.


MAKOSA 6 KWENYE HOTUBA YA RAIS KIKWETE KUHUSU(ESCROW)

Hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa leo ina makosa zaidi ya 100 niliyoweza kuya-identify haraka, haya sita. 
1. Rais hakupaswa kutoa ufafanuzi kuhusu pesa ni za umma au sio za umma. Ufafanuzi huo ulishatolewa na PAC, CAG etc.. Yeye alitakiwa kuwawajibisha wote waliotajwa kuhusika.

 2. Suala la Escrow hakupaswa kuongea na wazee ambao wengi walikuwa hawaelewi kinachojadiliwa na walikua wakisinzia tu. Angetaka kueleweka angezungumza na wasomi wa chuo kikuu cha Dar (UDSM) au chuo kikuu kingine chochote. 

3. Si kweli kuwa pesa za Escrow hazikuwa za umma kama Rais anavyojaribu kusema.

4. Ikiwa si pesa za umma kwanini amemfukuza Tibaijuka? Unawezaje kumfukuza mtumishi aliyechukua fedha binafsi "in good faith" 

5. Ikiwa si fedha za umma kwanini ameunda kamati ya kuchunguza waliotuhumiwa? Unawezaje kuwachunguza watu waliochukua hela binafsi. Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!

6.Sheria ya Utumishi wa umma inataka kiongozi wa serikali akipewa zawadi inayozidi sh.50,000/= aikabidhi kwa tume ya maadili ya viongozi.. Tibaijuka amepewa Bil.1.6 (zaidi ya mara 34,000 ya kiwango kilichowekwa na sheria). Lakini Tume hiyo haijaona kuwa hilo ni kosa na haikumchukulia hatua yoyote mama Tibaijuka hadi Rais Kikwete alipochukua hatua jana. Hii ina maana kuwa Rais ameisaidia Tume ya maadili kufanya kazi yake. Kazi iliyopaswa kufanywa na tume imefanywa na Rais mwenyewe. Huu ni udhaifu. This means Tume iliona ni sawa Tibaijuka kubeba hela kwenye sandarusi/rambo/viroba etc, ndio maana ilikaa kimya hadi Rais alipoona ni kosa. sasa jana ilitakiwa Rais Kikwete kabla hajamfukuza kazi Tibaijuka aivunje kwanza Tume ya Ma-deal maana imeshindwa kazi.!

MAJONZI TELE! FAMILIA YALA KRISMASI NJE!


Familia hiyo ikiwa nje baada ya nyumba yao kuvunjwa. Stori: Deogratius Mongela na Chande Abdallah
Familia moja yenye makazi yake Mtaa wa Mwembe-Madafu, Ukonga jijini Dar, imejikuta ikila Sikukuu ya Krismasi na kulala nje kwa madai kwamba nyumba yao imevunjwa na baada ya kuuzwa kwa mtu mwingine na mwanafamilia anayetajwa kwa jina la Omary Hamisi ambaye ni mtoto mkubwa wa familia hiyo. 
Akizungumza kwa masikitiko makubwa mbele ya waandishi wetu, mmoja wa wanafamilia hao, Rajabu Hamisi (28) alisema kuwa historia ya nyumba hiyo ilianzia pale baba yao, Hamis Mangandali alipopewa na mzee mmoja aliyemtaja kwa jina la moja la Kombo mwaka 1961. 
Rajabu alisema kwamba, migogoro ilianza mwaka 1991 baada ya Bibi Kombo Mbwana (mmoja wa wanafamilia ya Kombo) alipomkabidhi nyumba hiyo baba yake, Hassani Ali aliyetajwa kama babu yao mzaa mama. Alisema kuwa babu huyo aliiuza nyumba hiyo kwa mtoto huyo mkubwa wa mzee Hamisi aitwaye Omari Hamisi kwa kiasi cha shilingi elfu sabini (70,000/=) bila wanafamilia wengine kufahamu.Rajabu aliongeza kwamba, mwaka 2012, familia yao ilishangaa kupokea notisi ikiwataka wahame nyumba hiyo kwa muda wa siku 14 kwa kuwa ilikuwa tayari imeuzwa.

Baadhi ya vitu vya familia hiyo vikiwa nje. “Tulishangaa lakini hatukuwa na namna. Tuliendelea kuishi kwenye nyumba.
“Kweli baada ya siku kutimia walifika watu wakatutupia virago nje. 

“Walipoondoka tukarudisha vitu ndani na kuendelea kuishi lakini kwa wasiwasi,” alisema Rajabu ambaye alidai kuwa sekeseke hilo lilijitokeza mwanzoni mwa mwezi huu hadi sasa.Alisema ukiachilia mbali kutupiwa vitu nje, nyumba hiyo ilivunjwa kabisa huku ndugu yao aliyedaiwa kuiuza akitowekea kusikojulikana. 

“Hadi sasa familia yetu yote ipo nje, si watoto wala baba wote tunakaa nje, mvua yetu, jua letu. Kimsingi sisi hatuna cha sikukuu wala nini,” alisema Rajabu na kuongeza kuwa kwa kipindi chote hicho wamekuwa hawamuelewi ndugu yao ambaye ameuza nyumba hiyo kuwa ana nia gani na familia yao hasa baba yao ambaye ni mzee. 

TUME OPERESHENI TOKOMEZA KUKUSANYA MAONI MIKOA YA KASKAZINI NA KATI JANUARI 2015


Na. Mwandishi Wetu Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza  itakusanya taarifa na kupokea malalamiko yaliyotokana  na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili Nchini  mikoa ya Mikoa ya Arusha, Manyara, Tabora, Singida na  Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 24 Desemba,  2014 na Katibu wa Tume hiyo, Bw.Frederick Manyanda,  Tume inatarajiwa kuendelea na zoezi la kukusanya maoni  na taarifa kuanzia tarehe 5 Januari , 2015 mpaka tarehe 21 Januari,2015 katika maeneo mbalimbali ya kanda ya  Kaskazini na Kati Nchini.

Katika kutekeleza jukumu hilo, Bw. Manyanda ameeleza kuwa, Tume itatembelea Mkoa wa Tabora tarehe 4 Januari  2015 mpaka tarehe 8 Januari 2015 na itakuwa Mkoa  wa Singida tarehe 9 Januari,2015 mpaka tarehe 10 Januari,2015.

Aidha Tume itatembelea Mkoa wa Dodoma tarehe 11  Januari, 2015 mpaka tarehe 12 Januari 2015. Vilevile,  Wakili Manyanda ameeleza kuwa Tume itakusanya maoni 

Mkoa wa Manyara kuanzia tarehe 13 Januari, 2015 mpaka tarehe 16 Januari, 2015 na Tume itakuwa Mkoa wa Arusha tarehe 16 Januari 2015 mpaka tarehe 19 Januari,2015.

Mpaka sasa Tume ya Rais ya Operesheni Tokomeza imefanikiwa kukusanya taarifa na kupokea malamiko  yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza  katika mikoa kumi na tano (15) ya Tanzania Bara ambayo ni Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mwanza Mara,Lindi,Mtwara,Ruvuma,Iringa, Morogoro.Pamoja na mikutano hiyo, Bw. Manyanda ametumia fursa  hiyo kuwakumbusha na kuwaomba wananchi na watanzania  wa maeneo husika kuendelea kutuma taarifa na  malalamiko kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza  kwa njia ya barua, simu na barua pepe ambapo ameeleza  kuwa wananchi wanaweza kutuma barua kwa Katibu wa  Tume, Tume ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza  Ujangili, SLP 9050, Dar es Salaam na barua pepe kwenda  opereshenitokomeza@agctz.go.tz.Aidha, wananchi wa  maeneo husika wanaweza kutuma ujumbe mfupi wa  maandishi kwa namba za simu za Tigo: 0714 826826; 

Vodacom: 0767 826826; Airtel: 0787 826826; na Zantel:
0773 826826.

Jumatano, 24 Desemba 2014

MAKAMU MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA AKUTANA NA VIONGOZI WA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO WALIOPIGWA MABOMU JANA

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita Ambaye Pia ni Katibu Mkuu wa Pan African Union Ulio Chini ya Umoja wa Afrika AU  Anayehusika Kushugulikia Ajira kwa Vijana, Fursa ,Elimu Afya na Mambo yanayuwahusu Vijana Akiwasikiliza Kwa Makini Viongozi wa Mtandao wa wafanyabiashara Ndogondogo Kutoka Mkoani Dar Es salaam Aliokutana nao Leo Kusikiliza Changamoto zinazowakabili Vijana hasa Wafanyabiashara Ndogondogo  Maarufu Kama wamachinga walioipigwa Mabomu ya Mcahozi jana na Jeshi la polisi,Katika Kiako Hicho Viongozi wa wafanyabiashara Ndogondogo wameeleza Changamoto zinazowakabili kama Ukosefu wa Maeneo ya Kufanyia Biashara ,Kutokutambuliwa na Idara Yoyote ya serikali ,
Kutokusajiliwa .
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita  Amezichukua changamoto hizo kwenda kujadiliana na wadau mbalimbali kuona namna ya Kuzitatua ili Wafanyabiashara hao waweze kufanya biashara kwa uhuru na haki bila kubugudhiwa na watendaji  wachache wanaowatumia wafanyabiashara hao kwa maslai yao Binafsi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa wafanyabiashara Ndogondogo Kutoka Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Job Mwakatobe Akimweleza Mh Mhita Changamoto Kubwa Zinazowakabili wafanyabishara hao hali Iliyopelekea Sitofahamu Mpaka Kupigwa Mabomu ya Mcahozi jana
 Viongozi wanaounda Mtandao wa Umoja wa wafanyabiashara Ndogongodo wakijadiliana Jambo katika Kiakoa hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita  Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Viongozi hao leo Maraekanavyo. baada ya kuwasiliza na Kuchukua changamoto zianzowakabili wafanyabiashara hao kwa lengo la kwenda kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita  Akiwa na Viongozi wa Mtandao wa wafanyabiashara Ndogondogo Mkoani Dar es Salaam wakiwa Eneo la machinga Complex Kujionea hali hali mara baada ya Viongozi hao kumweleza ya kumwa Eneo Hilo lilijengwa Maalum kwajili ya wamachinga lakini cha kushangaza Wamepangishwa wafanyabiashara Wakubwa na Maofisi 
 Mh Mboni Mhita Akizungumza na Wafanyabiashara Ndogondogo aliotembelea Eneao hilo na kukuta Sehemu Kubwa Ikiwa Haina watu
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita  Akishuhudia Jengo Malum la Wafanyabiashara Ndogondogo la Machinga Complex likiwa Tupu wakati wafanyabiashara hao hawana Maeneo ya Kufanyiabishara ikielezwa Kwamba chanzo cha Jengo Hilo kuwa wazi ni Urasimu wa Namna ya Kupata eneo la Kufanyia Biashara

Maeneo ya wamachinga yakiwa katika Hali Mbaya Enewo la Ilala
Mh Mboni Mhita akishuhudia Mazingira Magumu ya Kufanyia Biashara.

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Mh Mboni Mhita  Akiagana na Viongozi wao wakipeana Mkakati wa namna ya Kutatua Changamoto zinazowakabili.
 
 
Blogger Templates