Social Icons

Jumatano, 30 Oktoba 2013

PATA PICHA MBALI MBALI ZA MECHI ILITIKISA TANZANIA JANA KATI YA MBEYA CITY AMBAYO IMEIBAMIZA 2-0 TANZANIA PRISONS.


Kikosi cha Mbeya City Fc wakiwa wanasali kabla ya Mechi yao kuanza 
 Kikosi cha Tanzania Prisons wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi kuanza 

 Hili Ni Benchi la Timu ya Mbeya City Fc Likiongozwa na Kocha mkuu wa Timu hiyo


Benchi la Tanzania Prisons 

Waamuzi wakiwa wanaamua timu ipi iianze mlango gani 
 Mashibiki wakiwa wanaingia uwanjani 
 Mashabiki wakiwa wanangoja mpira kwa hamu 




 Mashabiki wa Mbeya City Fc wakishangilia Goli la Kwanza 
 Mashabiki wa Mbeya City Fc wakishangilia Goli la Pili 
Mpira Unaendela ....
 Mpira umekwishaaa Wachezaji wa Mbeya City fc wakiwa wanashukuru kwa ushindi.. huku moja wa mashabiki akiwa anakimbizwa na Polisi 

 Wachezaji wa Mbeya City fc wakiwa wanashangilia Ushindi 
Hapatoshi Mashabiki wa Mbeya City Fc wakishangilia ushindi 

Jumanne, 29 Oktoba 2013

Pata picha,mazishi ya baba mzazi wa Wema Sepetu ni Jumatano hii ....Rais Kikwete na mama Salma watoa mkono wa pole



Balozi Isaac Abraham Sepetu ambaye ni baba yake mzazi na Wema Sepetu, anatarajiwa kuzikwa Jumatano hii visiwani Zanzibar. Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho asubuhi kuelekea visiwani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, leo wameungana na watu wengi wa karibu wa familia ya Wema kuwapa pole wafiwa akiwemo mama yake, Bi. Mariam Sepetu. 




Balozi Sepetu alifariki jana baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya kisukari na kiharusi na alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.



Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 





Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere hadi mauti inamfika; Mzee Sepetu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar




Angalia picha Watuhumiwa wa mauaji ya bilionea wa madini ya Tanzanite wa jijini Arusha wafikishwa mahakamani jana


Mshitakiwa, Sharif Mohamed Athuman (31), ambaye ni mshitakiwa namba

moja katika kesi ya Mauaji ya Bilionea wa Madini ya Tanzanite, Erasto
Msuya mchimbaji mdogo wa madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, muda mfupi baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka huu.
Mshitakiwa namba mbili, Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredi (38),

anayetuhumiwa na wengine saba, kumuua Mfanyabiashara Erasto Msuya kwa kumpiga risasi akitoka kwa taabu nje ya mahakama ya Hakimu mkazi
Moshi, baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka huu.
Mmoja wa Washtakiwa katika kesi ya Mauaji, anayetuhumiwa kushirikiana

na wenzake saba, kumuua Mfanyabiashara Erasto Msuya kwa kumpiga risasi akisindikizwa na Maaskari kutoka katika mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, muda mfupi baada ya kesi hiyo jana kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka huu.
Washitakiwa Joseph Damian "Chusa" na mwenzake Shaibu Jumanne Saidi

"Mredi", wakimsaidia Mshitakiwa mwenzao kupanda katika Gari la Polisi
muda mfupi baada ya kesi inayowakabili ya mauaji ya Bilionea wa Madini
ya Tanzanite, Erasto Msuya kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka
huu.

NAIBU WAZIRI WA MADINI AFUNGUA MAONESHO YA MADINI YA VITO ARUSHA,ATAKA USAWA WA KIBIASHARA.

Naibu Waziri wa Madini,Stephen Massele akiwasili kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha kufungua maonesho ya pili ya madini aina ya Vito yanayotoa fursa Tanzania kua kituo kikubwa kwa madini.
Naibu Waziri wa Madini,Stephen Masele akihutubia wadau wa madini leo kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha wakati akifungua maonesho ya pili ya madini aina ya Vito.
Wadu wa sekta ya madini kutoka ndani na nje ya nchi wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri Masele

Naibu Waziri wa Madini,Stephen Massele(kulia) akizungumza na mfanyabiashara madini nchini,Dk Anthony Frisby katika hoteli ya Mount Meru jijini.
Wafanyabiashara wakiangalia madini ya aina mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wa DRC
Naibu Waziri wa Madini,Stephen Massele akimsikiliza Mwenyeikiti wa TAMIDA,Sammy Mollel wakiti akitembelea mabanda ya wauzaji kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha ..
Madini ya Tanzanite ambayo huchimbwa nchini Tanzania pekee katika machimbo ya Mererani mkoa wa Manyara.

UN:Makali ya waasi wa M23 yamekwisha



Jeshi la serikali lineonekana hapa likiingia katika mji wa Rumangabo baada ya kuwafurusha waasi.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, ameambia baraza la usalama la Umoja huo kuwa makali ya kundi la waasi la M23 kama tisho la kijeshi yamekwisha

Martin Kobler alisema kuwa kundi hilo limeondoka katika maeneo yao ya kivita mashariki kwa DRC, na kwamba sasa wako katika eneo dogo karibu na mpaka wa Rwanda.
Waasi hao wanasema kuwa wameondoka katika maeneo yao ya vita kwa muda.
Aidha bwana Kobler aliambia baraza al usalama kupitia kwa njia ya Skype kuwa kwa sasa ni kama kundi ilo limefika mwisho wake.

Aliongeza kwamba waasi wameondoka katika ngome yao moja kuu ya mlima Hehu karibu na mpaka wa Rwanda.

Baada ya mkutano huo, balozi wa Ufaransa Gerard Araud alisema anatumai kutakuwa na mazungumzo sasa kati ya waasi hao na serikali.

Alisema: ‘‘Bwana Kobler ametuarifu kuwa wanashuhudia mwisho wa kundi la M23 kama tisho la kijeshi. Kwa hivyo naona kama ni hatua nzuri na kwamba hata kulikuwa na makubaliano kuwa sasa tushinikize mazungumzo kuanza tena mjini Kampala.’’

Mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi wa M23, mjini Kampala, yalisitishwa wiki jana.
Hali hata hivyo hali ilikuwa imetulia Mashariki mwa DRC kwa muda wa wiki moja.
Watu walionekana wakishangilia wakati wanajeshi walipoingia mji wa Rumangabo ambao ulikuwa umetekwa na waasi hao

Na sasa serikali inadhibiti hali mjini humo, kwa mujibu wa gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini, Julien Paluku.
‘‘Tumekuwa na mikutano miwili ili kujadili tutakavyoimarisha hali ya wananchi...na tutatangaza kuanza tena kutolewa kwa huduma za serikali katika muda wa masaa 24,’’ alisema Paluku.

Mji wa Rumangabo – ulio umbali wa kilomita 50 Kaskazini mwa Goma, mji rasmi wa Mashariki mwa DRC, ulikuwa na kambi tatu kubwa za kijeshi nchini humo kabla ya kutekwa na waasi wa M23 mwaka jana.
Hapana shaka kuwa majeshi ya serikali yamefikia hatua kubwa na kupata ushindi mkubwa dhidi ya waasi,

HISIA AZIDI KUPETA TUSKER PROJECT FAME: Angel ahitaji sapoti ya watanzania ili kuendelea kupeperusha bendera ya nchi yetu.


Baadhi ya washiriki wa shindano la Tusker Project Fame msimu wa sita wakisikiliza kwa makini maelekezo ya watangazaji wa kipindi hicho(hawapo pichani)kutoka kushoto ni mshiriki kutoka Tanzania Hisia, Hope kutoka Burundi na Bior kutoka Sudan ya Kusini
Mmoja wa washiriki kutoka Tanzania aliyeingizwa kikaangoni Angella Karashani(Angel)akimiliki jukwaa katika kipindi cha tatu cha Tusker Project Fame msimu wa sita huku akiimba kibao cha‘Don’t You Remember’ chake Adele Jumapili jijini Nairobi.
Mmoja wa washiriki wanaoiwakilisha vyema Tanzania Elisha Maghiya(Hisia)akimiliki jukwaa katika kipindi cha tatu cha Tusker Project Fame msimu wa sita huku akiimba kibao cha `Here I Stand’ chake Usher Jumapili jijini Nairobi.

28 Oktoba 2013, Ni baada ya vuta nikuvute katika kinyaganyiro cha shindano la vipaji vya kuimba maarufu kama Tusker Project Fame kipindi cha tatu ambapo kila mshiriki alikuwa amejinoa vya kutosha ili kuhakikisha anaendelea kubaki katika mashindano hayo. Wawakilishi wa nchi yetu Angel na Hisia walionekana kufanya vyema huku Hisia akipagawisha zaidi.

Mashindano yalianza huku kila mmoja akionesha kuwa na shauku kubwa hasa Bior, Fessy pamoja na Jennifer ambao walinusurika katika hatari ya kutolewa katika mashindano hayo baada ya kuwa wamerudia nyimbo zao siku ya jumamosi na kufanikiwa kubaki katika shindano hilo. Mishel kutoka Kenya pamoja na Under Coverbrothers kutoka Uganda waliaga mashindano hayo siku ya jumamosi.

Angel alimiliki jukwaa mara baada ya Patrick kufungua zoezi hilo. Akiwa amevalia gauni nyekundu iliyokuwa ikionesha wazi muonekano mzuri alionao huku ikimstiri vizuri aliimba wimbo wa ‘Don’t You Remember’ wa Adele. Alifanya vizuri huku akishangiliwa na mashabiki waliovutiwa na hisia zake katika kuimba wimbo huo. Majaji walionekana kutoridhirishwa sana na uimbaji wake wakimtaka aongeza jitihada kwani sauti ya kuimba anayo na anaweza, kikubwa ni kuongeza bidii.

Hisia nae alionyesha umahiri wake katika kuitumia sauti, kujiamini na kulimilliki vyema jukwaa baada ya kuutendea haki wimbo wa ‘Here I Stand’ wa Usher. Kutokana na kulitawala vyema jukwaa mashabiki walishindwa kujizuia hivyo wakaenda nae sambamba katika kuimba huku wakimshangilia na kuonesha kuwa hawana upinzani na uimbaji wake. Majaji nao hawakuwa na lakuongeza zaidi ya kumpongeza huku jaji Hermes akimpongeza kwa kumwambia kuwa Tanzania inajivunia uwepo wake katika mashindano haya. Pia mwalimu wa washiriki wa Tusker Project Fame Musyoka alimpogeza sana kwa kuyazingatia yale yote aliyofundishwa na kumtaka akaze kamba.

Wasanii wengine waliopagawisha ni pamoja na Bior mshiriki kutoka Sudani ya kusini ambae anapendwa sana na mashabiki na anaweza kulimili jukwaa vilivyo japo alikuwa katika hatari ya kutolewa na badae kujikomboa. Pia msanii Patrick aliyingia jukwaani na kibao cha I’m an African in New York’ cha Sting alionekana kuwabamba sana mashabiki na majaji hivyo kujihakikishia nafasi nzuri katika shindano hilo.

Mwisho wasanii wote walirudi jukwaani kwa pamoja ili kuvuna walichokipanda. Baada ya maelezo mafupi Jennifer alikuwa ni mshiriki wa kwanza kuchaguliwa kuwa katika hatari ya kutolewa huku ikiwa ni mara yake ya pili sasa kuwa katika hatari hiyo baada ya kunusurika katika kipindi kilichopita kwa kuokolewa na washiriki wenzake. Wa pili katika hatari hiyo alikuwa Angel mshiriki kutoka Tanzania ambae anahitaji sana kura zetu watanzania ili kuendelea kubaki katika mashinano hayo kwani uwezo wa kuimba anao. Wa tatu alikuwa ni Phionah kutoka Rwanda na wa mwisho alikuwa ni Fessy ambaye pia alirudi katika hatari kwa mara ya pili sasa.

Kabla ya onesho kuisha Dr Mich alimtambulisha mkurugenzi mpya wa muziki kwa wiki hii ambae ni jaji Hermes Bariki.

Meneja wa bia ya Tusker Sialouise Shayo kutoka katika kampuni ya bia ya Serengeti aliwashukuru sana na kuwapongeza washiriki Hisia na Angel kwa kuendelea kuiwakilisha vyema nchi yetu. Pia alisisitiza sana katika suala la kumpigia kura kwa wingi Angel kwani ana kipaji kikubwa na anaweza kusonga mbele kikubwa ni ushirikiano wa Watanzania katika kumuinua. Pia aliongeza kuwa kampuni hiyo ipo pamoja na watanzania katika kuhakikisha wanatuletea ushindi wa msimu huu.

Mpigie kura mshiriki Angel (Tusker 14) kutoka Tanzania ili aendelee kupeperusha bendere ya nchi yetu ili kumuwezesha kubakia katika shindano hilo. Usikose kufatilia moja kwa moja kipindi cha Tusker Project Fame msimu wa sita kupitia televisheni za EATV saa 2:00 usiku siku ya Juma mosi na saa 1:30 usiku siku ya Jumapili, pamoja na televisheni ya ITV kuanzia saa 4:00 usiku Juma mosi na Jumapili.


Kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako, haiuzwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.

Jumapili, 27 Oktoba 2013

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Kaskazini, kimemsimamisha Uongozi Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba


Taarifa ambazo tumezipata kutoka ndani ya kikao cha Baraza la uongozi kanda ya Kaskazini, kilichofanyika katika Hotel ya Corridor Spring leo usiku, zimedai uamuzi wa kusimamishwa Mwigamba umefikiwa na Kikao hicho baada ya kuwasilishwa kwa vielelezo kadhaa vya Mwigamba na yeye kukiri  kuwa ni vyake huku vingine vikimuonyesha kuwa ndiye mmiliki wa Akaunti ya Jina la ‘Maskini Mkulima’ ambalo limekuwa likitumika kukichafua chama kwenye mitandao ya kijamii.

  
Hakuna kiongozi ambaye amekuwa tayari kuzungumzia suala hili kiofisi, lakini taarifa za uhakika ambazo tumezipata kutokana  na maamuzi ya kikao hicho  zimebainisha kuwapo kwa maamuzi hayo pasipo shaka.
 
“Kikao hicho kimemsimamisha Uongozi kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili, hivyo kuanzia sasa mwigamba siyo kiongozi, nadhani tamko litatolewa baadaye,” alieleza mmoja wa wajumbe wa kikao  hicho kilichofanyika  Arusha na kuongeza kuwa katika Kompyuta yake baadhi ya maandiko ambayo yamekuwa yakikikashfu chama yamekutwa ikiwa ni pamoja IP address ya Jina na Maskini Mkulima ambalo limekuwa likituma post ndani ya Jamiiforums kukuta zinafanana.
 

Jina la ‘Maskini Mkulima’ lilijiunga na mtandao wa jamiiforums mnamo Desemba 27, 2011 na mpaka jana inaonyesha alikuwa ametuma zaidi ya Post 27 ikiwamo hii iliyokuwa na kicha cha habari: Wito kwa wana CHADEMA wote.
 
Makala hiyo ambayo ndiyo imefanikisha kumbaini ilitumwa Jamiiforums Oktoba 19 Mwaka huu chini ya kichwa cha habari cha ‘Wito kwa wana CHADEMA wote!’,inaeleza haya;
 

Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwa wana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wachama.

Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa matukio.
 
 Naandika nikiwa mwana CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Nimawasiliano baina yetu wana chadema na tunahitaji tutulie na kutafakari.
 
 Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika.

 Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake.
 
 CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wakamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC)kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake nini? 
 
 Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo?
 
 Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wakutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu. 

Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kila mwanachama.
 
 Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada ya hapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili.

 Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.
 
 Napenda pia kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani. 

Kakichukua kikiwa na wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49.

Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake CHADEMA imebeba agenda nzito za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa raslimali, katiba mpya,nk.
 
 Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye hakuna CHADEMA. 

Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao.
 
 Leo nitaainisha mambo machache tu yanayohusiana na fedha za chama na uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripoti za fedha wakajikuta wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata fursa:
 
 1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano. 

Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. 

Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama.
 
 Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. 

Kama kingekuwepo leo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi.

 Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe,  bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.
 
 2. Matumizi ya fedha za chama:
 
Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha.

 Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. 
 
 Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza kuu cha mwezi January kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa ipasavyo.
 
 Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna michango ya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. 

Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.
 
 3. Taarifa za fedha
 
Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za chama. 

Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu niliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. 

Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.
 
  4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama
 
 Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. 
 
Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya mchana. 

Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.
 
 5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi
 
 Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat. Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali kuzimwa.

 Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa katibu mkuu, hawana. 

Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari na pikipiki zote za M4C.
 
 Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni 80 ambazo mwenyekiti taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana. 

Na mwenyekiti anafanya mambo hayo yote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya kiutendaji ambayo yako chini ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na kamati yake ya tenda. Huu si ufisadi ni nini?
 
 6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama
 
Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya chama na chama kinanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya chama kama bendera vinauzwa na mtu binafsi. Jambo hili linajulikana kwa Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu wake tu. 

Napenda kwanza kuipongeza kamati ya bunge kwa kuvikomalia vyama vinavyopokea ruzuku bila kujali ni chama tawala ama pinzani.
 
 Pili namshauri CAG unaweza kutumia kampuni binafsi kwenye wizara, idara, taasisi, wakala, na asasi zote za kiserikali na serikali za mitaa kwenye ukaguzi lakini kamwe usiruhusu vyama vya siasa vikaguliwe na kampuni hizo. 

Hapo nenda mwenyewe ndo utajionea mwenyewe. Kampuni binafsi kwenye vyama huko zinafundishwa ziandikeje maoni yao. Nenda mwenyewe ujionee.
 
 Pia kuna mkakati unaendeshwa na CHADEMA Makao Makuu kwa sasa wa kuwapigia simu viongozi wa mikoa hasa hapa Dar es Salaam na mikoa mikubwa kama Mwanza, Arusha, Mbeya, nk, wakiwataka viongozi wa mikoani mtoe matamko kumpinga Zitto. Kataeni ushenzi huu. Hili si jambo la Zitto ni la kamati ya bunge na kimsingi ni la uadilifu ndani ya serikali na vyama. 
 
 Hata kama jambo lenyewe lingekuwa limeagizwa na Mwigulu Nchemba msingetoa matamko ya kupinga zaidi ya kuwaacha viongozi wetu wakuu watoe ripoti kuthibitisha uadilifu wao japo kidogo maana ni ukweli pia kwamba kwenye ripoti wanaweza kuzuga zikawa safi lakini ufisadi umefanyika. 
 
Kama ni matamko toeni matamko ya kuutaka uongozi wetu utoe hizo ripoti, na hapo ndipo mtakapo jua kwanini hampati ruzuku. Kuna matumizi mengi sana ya hovyo na ufisadi mkubwa unafanyika hapo Makao Makuu.
 
 Nitaendelea kuwadondolea ili muone kwa nini napendekeza tuung'oe uongozi huu chini ya Mbowe.
 
 
 
Blogger Templates