Phil Neville alisema msimu uliopita ulikuwa wa majanga kwa Manchester United chini ya David Moyes.
PHIL Neville amekiri kuwa kumteua David Moyes kuifundisha Manchester United lilikuwa janga kubwa.
Neville, ambaye aliteuliwa na Moyes kuwa kocha msaidizi namba moja msimu uliopita alisema: ‘Wote tulitakiwa kuwajibika, sio David Moyes tu. Niliwajibika na wengine waliohusika walitakiwa.
‘Mwaka uliopita ulikuwa ni janga kwelikweli, kuanzia mwanzo mpaka mwisho.’
Lakini Neville anaamini, United inaweza kurudi vizuri kutoka kwenye nafasi mbaya zaidi waliyomaliza ikiwa imepita miaka 24: ‘Nadhani tunaenda kushinda kombe,’ alisema. ‘Nafasi ya pili sio nzuri kabisa kwa Manchester United.
‘Tumepata nafasi nzuri mwaka huu kwasababu hatuna michuano ya Ulaya.
‘Ni kuwaunganisha pamoja na wachezaji wote wanaonekana kuwa tayari kushinda ligi tena baada ya kutoka kwenye maandalizi ya msimu’.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni