Wamekutana: Cristiano Ronaldo na James Rodriguez wakitoa dole kuashiria mambo 'supa' wakati wa mazoezi ya Real Madrid.
MWANASOKA BORA wa dunia, Cristiano Ronaldo amekutana na kijana mpya wa Real Madrid James Rodriguez katika mazoezi ya klabu hiyo mjini Madrid nchini Hispania.Rodriguez alijiunga na mabingwa hao wa Ulaya kutokea klabu ya Monaco kwa dau la paundi milioni 60 baada ya kuonesha kiwango kikubwa katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu na kutwaa kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa mashindano.
Ronaldo akifanya mazoezi katika uwanja wa Valdebebas
Ona kitu hicho: Nyota wa Real (kutoka kushoto) Ronaldo, Karim Benzema, Rodriguez na Raphael Varane wakati wa mazoezi ya Real Madrid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni