Mkubwa ukiendelea kuwaka katika eneo la juu la Jengo la Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Mivumoni (Mivumoni Islamic Seminary) iliyopo ndani ya Msikiti wa Mtambani,Kinondoni B Jijini Dar es Salaam leo.
Jitihada za kuuzima moto huo zimekuwa zikiendelea hadi hivi sasa,huku sehemu ya Waumini wa Kiislam wakijitokeza kwa wingi kusaidia juhudi hizo za kuuzima moto huo zilizokuwa zikiendesha na Kampuni ya Kuzima moto ya Ultimate,japo baadae gari hilo liliisha maji,hali iliyowapelekea Waumini hao kulijaza maji gari hilo kwa kutumia ndoo huku kazi ya Uzimaji moto huo ikiendelea.
Chanzo cha Moto huo,inadaiwa ni hitilafu ya Umeme iliyokuwepo kwenye Bweni la Wasichana Wanafunzi wa Shule hiyo.Hakuna mtu yeyote aliepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo.Picha zote na Othman Michuzi.
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka kwenye eneo hilo.
Ulinzi mkali wa Polisi ulitawala katika eneo la Msikiti huo wa Mtambani kuhakikisha Usalama unakuwepo kwenye eneo hilo.
Sehemu ya Waumini wa Kiislam wakishirikiana kusombelea maji ili kuuzima moto huo.
Jitihada zikiendelea.
Gari la Zima Moto mali ya Kampuni ya Ultimate Security likijazwa maji kwa ndoo ili kuendelea na zoezi la uzimaji w amoto huo.
Likafika na gari hili kwa ajili ya kusaidia kuzima moto huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni