Social Icons

Jumapili, 10 Agosti 2014

MAN UNITED WAPIGWA BAO VERMAELEN ATUA RASMI FC BARCELONA.

Rasmi: Thomas Vermaelen ametua Barcelona baada ya Asrenal kugoma kuwauzia silaha Man United

Naodha wa Arsenal, Thomas Vermaelen amejiunga na Barcelona kwa dau la Pauni Milioni 15 baada ya timu hiyo ya Kaskazini mwa London kugoma kuwauzia silaha wapinzani wa Ligi Kuu England, Manchester United.
Beki huyo Mbelgiji amesaini Mkataba wa miaka mitano na vigogo hao wa Hispania, ambao unaaminika utamfanya awe analipwa Pauni 80,000 kwa wiki.
Vermaelen amekuwa Arsenal kwa miaka mitano na miaka miwili akiwa Nahodha wa kikosi cha Arsene Wenger, lakini msimu uliopita alijikuta anawekwa benchi Laurent Koscielny na Per Mertesacker.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates