Social Icons

Jumatatu, 4 Agosti 2014

CCM YADAIWA KUKODISHA WATU KWENYE MDAHALO KWA AJILI YA KUWAZOMEA UKAWA NA KUWASHANGILIA WANAOUNGA MKONO SERIKALI MBILI





picha za watu wanaodaiwa kukodiwa wakishuka kutoka katika moja ya mabasi ya UDA

Habari ambazo zimeifikia hivi punde zinasema kwamba ,chama kimoja cha siasa kimetoa zaidi ya shilingi milioni 5 kwa ajili ya kukodisha watu watakaokuwa na kazi kubwa ya kuwazomea watoa mada zenye mtazamo wa kuunga mkono serikali 3,kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari vijana hao walikodiwa kutoka maeneo ya vingunguti,Buguruni na maeneo mengine ya jiji la Daresalam,
Habari zaidi zinasema,chama hicho kimefikia hatua hiyo baada ya kuona midahalo iliyofanyika jana na siku 3 nyuma ziliweza kubadili fikra na mitazamo ya jamii juu ya serikali 3,hivyo kuazimia kuuteka mdahalo wa leo uliofanyikia katika ukumbi wa Nkurumah uliopo chuo kikuu cha Daresalam,imetajwa kwamba kazi kuu ya watu hao itakuwa ni kuwashangilia watoa mada na wachangiaji mada wale wanaounga mkono muundo wa serikali 2 na  .

Mdahalo huo ambao umeandaliwa kwa kiasi kikubwa na chama hicho kinachounga mkono serikali 2 kwa kupitia kwa uongozi wa chuo kikuu hicho UDASA,huku kiongozi mmoja wa UDASA akitajwa kupita kuwashawishi watu mbalimbali kuanzia wakufunzi na wasomi wanaopatikana jijini Daresaalamu na mjini Morogoro,
FEDHA ZAMWAGWA KWA WATAKAOTEKELEZA ZOEZI LA ZOMEA ZOMEA
Mtoa habari wetu anadai katika kiwango hicho cha shilingi milioni 5 washangilia na wazomeaji hao maalumu wamelipwa kuanzia shilingi elfu 5000 mpaka shilingi elfu 50000 kutokana na uzito wa mhusika.

MAKADA WA CCM WATAJWA

Mtoa habari wetu ambaye alikataa kutaja jina lake alienda mbali kwa kuwataja kwa majina watu wawili aliodai kwamba ni makada wa CCM,na aliwataja kwa  jina 1 moja ,akimtaja Wasi,Madel na Tibai,kwamba watajwa hapo juu ndo waliratibu zoezi zima la ufanikishwaji wa zoezi zima,kuanzia kuwatafuta watu na kuwafikisha ukumbini na ndio walioratibu zoezi la ugawaji na upangwaji wa viwango vya malipo.

UDA YAHUSISHWA

Kampuni ya Usafirishaji jijini Daresaalam UDA ambayo katika siku za hivi karibuni iliingia katika mgogoro mkubwa wa umiliki wake,ndio kampuni iliyotajwa kutoa mabasi yake kuwasafirisha watu hao mpaka eneo la mkutano ambao utafanyikia kwa makubaliano fulani ambayo bado mtoa taarifa wetu ameahidi kufuatilia na kutuletea taarifa kamili.

"Lengo kuu likiwa ni kuhakikisha hoja za watoa mada wa UKAWA hazisikilizwi wala kupewa umakini"alimaliza kusema mtoa mada wetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates