Mwanaume mmoja anazuiliwa na polisi nchini Uingereza kwa kutoa tahadhari gushi kuhusu kuwepo kwa bomu katika ndege ya Qatar iliyokuwa ikitoka Doha kuelekea Manchester nchini Uingereza.
Ilikuwa kihoja na taharuki kwa mamia ya jamaa na marafifki wa abiria waliokuwa katika ndege hiyo ambayo ilisindikizwa na ndege za kijeshi hadi kwenye uwanja wa ndege wa Manchester.
Ndege zote zilizokuwa zinatarajiwa kutua ama kuondoka kutoka uwanjani humo zikilazimika kusubiri ama kuelekezwa kutua kwengineko kwa takriban nusu saa.
Kulingana na rubani wa ndege hiyo,alipokea ujumbe kutoka kwa abiria moja ikidai kulikuwemo kilipuzi katika ndege hiyo.
Polisi waliingia ndani ya ndege hiyo na kumkamata abiria mmoja mwenye umri wa miaka 47 .
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 269 na wahudumu 13 inamilikiwa na shirika la ndege la Qatar aina ya Airbus A330-30
Polisi wa mji wa Manchester walimkamata bwana huyo anayetokea maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Manchester.
Abiria mwenza Josh Hartley, aliyekuwa anasafiri kutoka Doha Qatar anasema ilikuwa tukio la kushtua sana maanake hawakutarajia kusindikizwa na ndege za kijeshi .
''ndege za kijeshi ndizo zilitubabaisha sana niliogopa sana''.
Taarifa kutoka kwa shirika hilo la ndege ilisema kuwa ndege hiyo QR23ilitua bila ya matukio katika uwanja wa ndege wa Manchester .
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa ''Wahudumu wa ndege hiyo walipata taarifa kutoka kwa abiria kuwa kulikuwa na kilipuzi ndani ya ndege hiyo na wakachukua tahadhari na kuwaarifu maafisa wa usalama wa anga nchini Uingereza.
''Wahudumu wa ndege hiyo wanaendelea kushirikiana na maafisa wanaochunguza tukio hilo.''
Ndege 9 zilizoratibiwa kutua katika uwanja huo wa Manchester zilitumwa katika viwanja mbadala 5 zikilazimika kutua katika uwanja wa Leeds Bradford .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni