Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu akizingirwa na washabiki.
Hali ya kushangaza watu mbalimbali ambao ni mashabiki wa msanii wa filamu, Wema Sepetu walizingira gari la staa huyo huku wakimuamuru ashuke ili akaungane na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Tukio hilo lilitokea Jumatano hii maeneo ya Sinza-Mori, jijini Dar ambapo ndipo kulikuwa kikomo cha msafara uliokwenda kumpokea Diamond Uwanja wa Ndege Julius Nyere, Dar baada ya kutua akitokea kwenye tuzo za Afrimma, mashabiki hao walilizingira gari la mwanadada huyo huku wakimtaka Wema atoke ndani ya gari akapande kwenye gari alilokuwepo mpenzi wake huyo, wapigwe picha lakini hakushuka.
“Tunamtaka Wema ashuke kwenye gari lake apande huku kwa Diamond akae naye pale juu tuwashangilie kwa pamoja la sivyo hatupishi, tutaendelea kulizingira,” walisikika wakilalama mashabiki hao kwa nyakat tofauti, licha ya Wema kukataa kushuka, baadaye wakatulia na kuachia msafara uendelee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni