Social Icons

Jumamosi, 16 Agosti 2014

JAJI WEREMA APINGANA NA IKULU ,ASEMA BILA UKAWA HAKUNA KATIBA


IMG_0173Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akitoa ufafanuzi wa masuala Kisheria kwa waandishi wa habari kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
IMG_0197Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akiwaonesha waandishi wa habari Rasimu ya katiba wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria katika mchakato wa Katiba wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam 
IMG_0199
IMG_0206
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa vyama vya siasa waliopo nje ya Bunge Maalumu la Katiba wameaswa kurejea bungeni ili kufanya maridhiano ndani ya bunge hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.
Jaji Werema amesema kuwa wajumbe walio nje ya Bunge Maalum hawana budi kurejea bungeni na kuacha kumshinikiza Rais kulivunja bunge hilo kwani hana mamlaka ya kulivunja kulingana na sheria inayoliongoza bunge hilo.
“Sheria inasema kuwa baada ya bunge hilo linaweza kuvujwa baada ya katiba kupatikana, kinyume na hapo bunge husitishwa kufikia maridhiano na kufikia mwafaka kwa kufuata misingi ya demokrasia.” alisema Jaji Werema.
Pia Jaji Werema alisema kuwa wajumbe walio nje ya bunge hilo hawana budi kurudi ili kuendelea kujadili vipengele vingine vya rasimu ili kuweza kupata katiba iliyo bora kwa nchi na watu wake.
Aidha, Jaji Werema aliviasa vyombo habari kutumia nafasi yao ya kuwa mhimili muhimu katika uongozaji wa nchi kutokuwa na upendeleo katika utoaji wa taarifa na kuacha kuongozwa na mawazo ya wachache ili kuweza kusaidia nchi kupata Katiba Mpya kwa manufaa na maendeleo ya nchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates