Bado nipo nipo kwanza!: Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema, ameamua kuongeza mkataba mpaka mwaka 2019.
KARIM Benzema ameamua kuzeekea Real Madrid baada ya kuongeza mkataba wake mpaka mwaka 2019.Nyota huyu alikuwa anahusishwa kujiunga na baadhi ya klabu za ligi kuu, lakini biashara imekatika ghafla na sasa Mfaransa huyo ataendelea kudunda dunda Santiago Bernabeu.Arsenal, Liverpool na Tottenham Hotspur zilikuwa miongoni mwa klabu nyingi za ligi kuu England zilizokuwa zikihusishwa kumsajili mshambuliaji huyo mwenye miaka 26, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Lyon hatafanya baishara ya kucheza England msimu ujao.
Aliwindwa: Benzema alihusishwa kujiunga na klabu za Liverpool, Tottenham au Arsenal majira haya ya kiangazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni