Watu walioishi katika ndoa kwa miaka 62 wamekufa pamoja nchini Marekani. Don na Maxine Simpson, kutoka Bakersfield, California walipishana kwa saa chache tu kufa, katika vitanda vilivyowekwa karibu, huku wakishikana mikono katika saa zao za mwisho duniani.
Melissa Sloan, ambaye ni mjukuu, amesema bibi yake alitangulia kufa, na mwili wake ulipoondolewa chumbani, babu yake naye akafuata.
"Kitu pekee alichokitaka Don ni kuwa na mke wake mpenzi. Alimpenda sana bibi yangu, mpaka mwisho”
Don alikuwa na umri wa miaka 90, huku Maxine akiwa na miaka 87. Walikutana mwaka 1952 na kuoana mwaka huohuo.
Wawili hao waliwahi kuishi nchini Ujerumani wakati Don akifanya kazi katika jeshi la Marekani kama mhandisi, na walipokuwa huko, wali-asili watoto mapacha wa kiume kutoka katika nyumba moja ya kulelea watoto yatima.
Waliporejea Marekani, Maxine alifanya kazi ya uuguzi huku Don akifungua kampuni yake ya uhandisi.
Wameacha mtoto mmoja wa kiume na wajukuu watano
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni