Social Icons

Ijumaa, 29 Agosti 2014

MAGAZETI YA LEO

1_0e849.jpg
27_7eb6d.jpg
3_965cf.jpg
26_758bc.jpg
4_4f685.jpg
026_890d1.jpg
2_98cb7.jpg
25_17eb5.jpg
5_9563d.jpg
027_14284.jpg
10_0599f.jpg
35_8fad0.jpg
11_c5a36.jpg
36_822ec.jpg
12_cb284.jpg
37_dbe67.jpg
64_2e431.jpg
65_675c7.jpg
66_43796.jpg
67_635a9.jpg

ANGALIA PICHA MTOTO WA MIAKA 9 ALIVYOMUUA MWALIMU WAKE

Hii ni sehemu ya video ya mfunzo hayo kabla ya tukio. 
Pale ambapo kwanza unaweza kushtushwa na umri mdogo wa mtoto mwenyewe aliyekua anafundishwa kufyetua risasi kwenye bunduki, hii imetokea Arizona nchini Marekani ambapo mtoto wa miaka 9 ndio kichwa cha habari kwenye mafunzo ya kutumia submachine gun iliyotengenezwa Israel.


Mtoto huyu wa kike anaetokea New York alikua kwenye mapumziko na matembezi kama mtalii kwenye mji wa Arizona ambako pia ndio alichukua time yake ya ziada kujifunza kutumia bunduki lakini kwa bahati mbaya risasi ikafyetuka na kumjeruhi mwalimu wake aitwae Charles Vacca mwenye umri wa miaka 39 ambae alifariki baadae hospitalini.
Wakati tukio linatokea mtoto huyu alikua na wazazi wake ambapo tovuti ya bullets and burgers imesema watoto kati ya miaka 8 na 17 wanaweza kufyetua risasi kama iwapo tu watakua chini ya uangalizi wa Mzazi au Mwalimu.

Hii sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili, ilishawahi kutokea mwaka 2008 ambapo mtoto wa miaka 8 alijiua kwa bahati mbaya kwa risasi kwenye onyesho la bunduki hukohuko Marekani.

KAMPUNI YA MATANGAZO YANAYOTEMBEA (TRIA) YAZINDULIWA RASMI TANZANIA

DIANA LAVENDER Meneja Mauzo na Masoko kampuni ya CONICA MINOLTA akisoma risala yake wakati wa uzinduzi wa matangazo hayo.
TRUSHAR KHETIA Mkurugenzi Mtendaji wa TRIA akikata utepe wakati akizindua rasmi matangazo hayo nchini Tanzania, wa pili kulia ni ZULFIKAR MOHAMED Meneja Mkuu wa kampuni ya TRANSPAPER EXPRESS na mwisho kulia ni DIANA LAVENDER Meneja Mauzo na Masoko kampuni ya CONICA MINOLTA na kushoto ni AZDA AMANI Meneja wa Huduma Shirika la ndege la PRECISION AIRLINE ambao ni wateja wa kampuni ya TRIA.

Kampuni ya matangazo kwa kutumia vifaa tembezi yaani matangazo yanayotembea imezinduliwa rasmi jijini Dar esSalaam.

Akiongea na waandishi wa habari pamoja na wageniwengine waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi ulifanyika katika hanga la shirika la ndege la Precision yenye makao makuu yake eneo la uwanja wa ndege jijini Dar esSalaam, mkurugenzi mtendaji na muasisi wa TRIA bw. Trushar Khetia amesema kuwa TRIA ni kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na matangazo yawekwayo juu, nje au ndani ya fifaa safirishi kama mabasi ya kusafiria ndani na nje ya miji, ndege na usafiri wa majini maarufu kama boti au meli.

“Tumezoea kuona ama kusikia matangazo malimbali ya kibiashara nay ale ya kijamii yaani matangazo yasiyo ya kibiashara yakifanyika kupitia kwenye TV REDIO magazeti na majarida hapa nchini lakini leo TRIA inawathibishia wafanya biashara wa Tanzania na wengine kuwa matangazo yanaweza kufanyika popote wakati wowote tena kwa gharama ndogo” alisema bwana Trushar na kuongeza kuwa TRIA ina lenga kuwainua watanzania hasa vijana wadogo na kuwafanya watambue fursa zao katika maisha sambamba na kuwaongezea matumaini makubwa wamiliki wa mabasi, ndege, daladala namakapuni ya usafirishaji katika kunufaika kutokana na biashara zao za usafirishaji.

Aidha bwana Trushar amesema kuwa kampuni yake pamoja na kwamba haitegemi kufanya biashara kwa hasara hailengi pia kutengeneza faida tu bali kuleta ufanisi na changamoto endelevu katika sekta ya masoko na matangazo ambapo vijana wadau na wateja wa huduma hiyo wataweza kupiga hatua za kimaendeleo kibiashara sambamba na kuongezeka kwa soko la ajira hususana kwa vijana wa kitanzania “TRIA Tanzania hailengi kutengeneza faida tu bali pia kuleta maendeleo yenye tija kibiashara kwa wale watakaokuwa wateja wetu na wadau kwa ujmla, lakini pia ajira kwa vijana wenye uwezo tofauti tofauti wa kufanya kazi pamoja na wale wenye utaalamu wa kuandaa na kutengeneza matangazo haya” alisema Khetia.

Kwa upande wake mwakili wa Conica katika hafla hiyo Bi Diana Lavender amesema Conoca imekuwa mteja mkubwa wa TRIA nchini Kenya na kwakutambua ubora wa kazi zinafanywa naTRIA Conica imeamua kuunga na TRIA kwakuendelea kufanya matangazo yake hapa chini “tumekuwa wateja wa hii kampuni mda mrefu sasa huko nchini Kenya na kutoka na mafanikio makubwa tumeweza kupata kupitia matangazo yetu yanayofanywa na TRIA tumeonelea kuwa ni vizuri kuja kufanya hayo matangazo hapa Tanzania hasa pale tuliposikia kwamba TRIA inaanzisha tawi hapa nchini” alisema Lavender na kuongeza kuwa kufanya matangazo kupitia mabasi, ndege, daladala, treni, vyombo vya usafiri wa majini ni sehemu ya mapambo ya mji na njia zake kwani matangazo haya hutengenezwa vizuri na kufanya kuvuta macho ya wengi kila ipitapo “ni ma mabasi yetu huko Kenya maarufu kama matatu ukipita ukiona vile inavutia lazima utafurahia na kwamba lazima unaweza kutaka kupanda hiyo basi” aliongeza.

Naye mwakilishi kutoka shirika la ndege la precision hapa nchini ambao ni moja kati ya wadau wa karibu kabisa na TRIA Bi Azda Amani amesema kuwa uwekezaji wa biashara mbalimbali hasa biashara ngeni kama hayo ni sehemu ya kuongeza na kukuza pato la taifa na kupitia kodi kwa kampuni husika lakini pia kwa wamiliki wa mabasi, ndege na vinginevyo pamoja na wale wamiliki wa matangazo yatakawekwa kwenye magari haya watalipia kodi “ni furaha kuona wawekezaji wakubwa na wadogo wakiingia kila siku hapa nchini kuwekeza kibiashara na kwakufanya hivi nchi yetu ina kuwa pia kiuchumi kupitia kodi kutoka kwa watoa huduma na wahudumiwa wa huduma hii muhimu kwa maendeleo ya uchumi na biashara nchini” alisema Amani

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Zulfikar Mohamed kutoka Transpaper ameisifia TRIA kwa hatua iliyofikia na kuwataka watanzania kuiga mfano huo muhimu na kwenda kuwekeza pia katika nchi jirani hata kimataifa “ mimi nipewa fursa ya kuzindua tawi la TRIA hapa Tanzania na kwakweli nimefurahia fursa hii.

Naomba kuwapongeza sana wahusika wote waliokaa na kuona kwamba mimi naweza kuwa mgeni rasmi wa kuzindua mradi huu muhimu lakini pia nawasifia watanzania kwa kuwa waungwana wakubwa sana kuwapokea wawekezaji kutoka pande zote za dunia bila kujali rangi kabila wa udini, kwa hili mko vizuri sana na nawapongeza sana niwaombe tu kwamba igeni huu mfano mzuri na nyinyi mkawekeze biashara zenu katika nchi nyingine kwa manufaa ya watoto wenu na watanzania wote” alisema Mohamed nakuongeza kuwa maendele ya kiuchumi katka taifa lolote huletwa na wenye nchi kupitia biashara yenye tija na inayovuka mipaka na kuleta fedha za kigeni.

WATU ZAIDI YA KUMI WAFARIKI KATIKA AJALI MBALIZI MBEYA








XABI ALONSO ATUA UJERUMANI KUSAINI BAYERN MUNICH

 Kiungo Xabi Alonso ametua jijini Munich, Ujerumani tayari kufanya vipimo na baadaye kumalizana na Bayern Munich.


Alonso anatarajia kujiunga na Bayern kwa kitita cha pauni milioni 7.5.
Kiungo huyo mkabaji mwenye miaka 32 alijumuika na mashabiki kwa kusaini autograph kuonyesha tayari amewasili na atakuwa nao.

Alhamisi, 28 Agosti 2014

ROJO APATA KIBALI CHA KUFANYA KAZI NCHINI ENGLAND


Photo: Marcos Rojo amapata kibali cha kufanya kazi nchini England na ilitegemewa jumamosi hii aanze kuitumikia United lakini taarifa kutoka UK zinasema kwamba mchezaji huyo wa kiargentina anaweza bado asipate ruhusa ya kuichezea klabu mpya kutokana na ugomvi wa kisheria uliopo kati ya Sporting Lisbon na kampuni ya Doyen Sports iliyokuwa inamiliki haki zake za usajili kwa asilimia 75. 
United imemsajili Rojo kutoka Lisbon kwa ada ya jumla ya £16m lakini wamelipa £8m kwa sasa na baada watalipa £4m X2. Premier League hairuhusu suala la 'umiliki wa pande 3' (Third Part Ownership) - mtindo ambao unaruhusiwa kwenye nchi kama Ureno alipotoka Rojo. Tatizo la Third Part Ownership liliwahi kuiletea matatizo West Ham huko nyuma waliposajili Carlos Tevez na  Javier Alejandro Mascherano
Marcos Rojo amapata kibali cha kufanya kazi nchini England na ilitegemewa jumamosi hii aanze kuitumikia United lakini taarifa kutoka UK zinasema kwamba mchezaji huyo wa kiargentina anaweza bado asipate ruhusa ya kuichezea klabu mpya kutokana na ugomvi wa kisheria uliopo kati ya Sporting Lisbon na kampuni ya Doyen Sports iliyokuwa inamiliki haki zake za usajili kwa asilimia 75. 

United imemsajili Rojo kutoka Lisbon kwa ada ya jumla ya £16m lakini wamelipa £8m kwa sasa na baada watalipa £4m X2. Premier League hairuhusu suala la 'umiliki wa pande 3' (Third Part Ownership) - mtindo ambao unaruhusiwa kwenye nchi kama Ureno alipotoka Rojo. Tatizo la Third Part Ownership liliwahi kuiletea matatizo West Ham huko nyuma waliposajili Carlos Tevez na Javier Alejandro Mascherano

PRODYUZA SUGE KNIGHT ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI


Prodyuza Suge Knight wakati akiwasili katika klabu ya usiku ya 1Oak ambapo baadaye alishambuliwa kwa kupigwa risasi sita.
 PRODYUZA Suge Knight ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Cedars-Sinai, Los Angeles nchini Marekani alipokuwa amelazwa baada ya kujeruhiwa kwa risasi katika klabu ya usiku ya 1Oak kwenye pati ya utangulizi wa utoaji Tuzo za VMA Jumamosi usiku.
 
Mmoja wa majeruhi katika shambulio hilo akipatiwa huduma ya kwanza.
 Suge aliruhusiwa jana na ataendelea na matibabu madogomadogo akiwa nyumbani kwake. 

Mbali na kujeruhiwa, Suge anadaiwa kutotoa ushirikiano kwa polisi kuhusu tukio hilo lililotokea katika pati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mwanamuziki Cris Brown anayedaiwa kuwa ndiye alikuwa mlengwa mkuu wa shambulio hilo.
 
 Mwanamitindo Megan Hawkins akiwa hospitali ya Cedars-Sinai baada ya kujeruhiwa kwenye shambulio hilo.
 Suge alipigwa risasi sita, nne tumboni, moja kifuani na nyingine mkononi ambapo watu wengine wawili akiwemo mwanamitindo Megan Hawkins nao walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Cedars-Sinai kwa matibabu.

MAGAZETI YA LEO



Tozz Kibonge



Happy bith day Tozzz kibonge Jabir Salehe frome Times Fm 100.5

Jumatatu, 25 Agosti 2014

BARCA YAUA 3-0 LA LIGA,PAKA JEUSI LAKATIZA UWANJANI CAMP NOU


Paka mweusi akikatiza Uwanja wa Camp Nou janaBARCELONA imeanza vyema La Liga kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Elche Uwanja wa Camp Npu usiku wa kuamkia leo.Katika mchezo huo, kiungo wa Barca Javier Mascherano alitolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza, kocha mpya Luis Enrique akiiongoza timu kwa mara ya kwanza, alionyesha mwanzo mzuri.
Mchezaji wa timu gani? Paka huyu alisababisha mechi isimame ili kwanza apite
Lionel Messi kushoto akifurahia baada ya kufunga mabao mawili
Lionel Messi aliifungia Barca bao la kwanza baada ya kuwazidi ujanja mabeki sita Elche, kabla ya kinda Munir El Hadaddi kufunga la pili, mabao yote kipindi cha kwanza. 
Nyota wa Argentina, Lionel Messi alifunga bao lake la pili na la tatu la kuhitimisha ushindi wa Barca baada ya jitihada binafsi kipindi cha pili.
Paka mweusi alikatiza Uwanja wa Camp Nou mwanzoni tu mwa mchezo na kusababisha mechi isimame kwa muda ili aondo

WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO

 Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
 Kikundi cha ngoma kikitumbuiza mara baada ya kuwasili kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
 Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akigawa fulana maalum zenye nembo ya TANAPA na Real Madrid kwa mmoja wa wachezaji kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
 Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Erastus Lufungulo akitoa neno la ukaribisho kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid walipowasili kwa ziara fupi. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Elinas Palangyo, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bi. Devota Mdachi, Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete na Afisa Utalii Antipas Mgungusi.
 Wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid pamoja na wenzi wao wakiwa Hifadhi ya Kilimanjaro.
 Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani) akiongoza msafara wa wakongwe wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro
Wakongwe wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro
 Eneo la Maporomoko ya Maji ambapo wachezaji wakongwe wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani Kilimanjaro.
 Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa cheti cha ushiriki kwa mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakongwe wa Klabu ya Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
 
 
Blogger Templates