Uchaguzi wa wabunge Swaziland
Wapiga kura nchini Swaziland wanawachagua wabunge wapya. Nchi
hiyo ina ufalme mdogo uliosalia Kusini mwa Afrika unaoongozwa na mfalme Mswati
wa tatu.
Vyama vya kisiasa havijaharamishwa nchini humo, lakini vimedhibitiwa na
ufalme huo. Wagombea wa nafasi za wabunge wa bunge lenye wanachama wa 55,
wanachaguliwa na viongozi wa kitamaduni wanaomuunga mkono mfalme.
Wakosoaji wamepuuzilia mbali uchaguzi huo na kusema ni njia moja ya kuendelea
kuidhinisha utawala wa mfalme. Hii ni licha ya baadhi ya watu wanaounga mkono
mageuzi pia kuchaguliwa kwenye bunge hilo.
Changamoto kuu kwa ufalme itakuwa kukabiliana na viwango vya umaskini pamoja
na upungufu pesa za matumizi ya serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni