Zaidi ya watu 300 wamejeruhiwa
Tetemeko kubwa la ardhi limewauwa watu 270 katika mkoa wa
Kusini Magharibi wa Balochistan nchini Pakistan.
Tetemeko hilo la kipimo cha 7.7-lilipiga Jumaanne alasiri . Nyumba nyingi
zilibomolewa na watu wengi walipaswa kulala nje.
Baada ya tetemeko hilo ,kisiwa kidogo kiliibuka nje ya mwambao karibu na
bandari ya Gwadar.
Watu walikusanyika ufukweni kushuhudia kisiwa hicho kipya ambacho
kinakadiriwa kua na urefu wa mita 200 na upana wa mita 100 na kiinuka mita 20
kutoka upeo wa bahari .
Balochistan ndio mkoa mkubwa wa Pakistan lakini ukiwa na watu wakaazi
wachache kupita yote
Eneo hilo hukumbwa na mitetemeko ya mara kwa mara na mnamo mwezi wa Aprili
watu 35 waliuwawa katika tetemeko ambalo kitovu chake kilikua Kusini Mashariki
mwa Iran mnamo mwezi wa April.
Vibanda vya udongoTetemeko hilo lilikua la nguvu hata watu wa miji iliyo mbali ya Karachi,
Hyderabad, na mji mkuu wa India, Delhi walihisi mtikisiko wake.Vijiji vizima inaarifiwa vilifyekwa katika wilaya ya wakaazi masikini ya
AwaranMsemaji wa serikali ya Balochistan, Jan Buledi,
Amesema waliopatwa na maafa
zaidi ni katika mji wa Awaran na vijiji vinavyouzingira na ameonya idadi ya vifo
huenda ikaongezeka. Takriban watu 340 wamejeruhiwa.Msemaji huyo amesema kuna ukosefu mkubwa wa huduma za matibabu na hospitali
hazina nafasi za kutosha kuwatibu majeruhi .Alisema helikopta zinawasafirisha majeruhi mahututi hadi mjini Karachi na
wengine wanahudumiwa katika wilaya jirani.
Jeshi la Pakistan lilikua miongoni mwa makundi ya kwanza kutoa msaada kwa kua
tayari limekua huko miaka kadhaa sasa kwa sababu ya uasi wa watu wanaotaka
kujitenga kwa mkoa huo wa Balochistan.Jeshi limesema limetuma zaidi ya wanajeshi 200 , wana matibabu na mahema
kutoka mji mkuu wa mkoa huo Quetta, lakini shughuli za uokozi zinatatizwa kwa
hali ya milima ya eneo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni