PATA PICHA NA HABARI ZA TUKIO LA UVAMIZI WA JENGO LA KIBIASHARA WESTGATE MALL NAIROBI,KENYA.MPAKA SASA NATOA HABARI HII BADO WAVAMIAJI HAO HAWAJATOKA KATIKA JENGO HILO NA WALA HAWAJAKAMATWA.
Hali ni tete katika jiji la Nairobi ambapo washambuliaji wenye silaha
wamevamia eneo la kifahari la Westgate Mall nje kidogo ya jiji la
Nairobi.
Vyombo vya habari vya Kenya vinaripoti kuwa washambuliaji hao waliokuwa wamegubika nyuso zao walivamia maduka hayo mwendo wa saa sita mchana kwa saa za Kenya na kuwateka nyara watu kadha.
Wafanyakazi wengi wamenaswa katika mtafaruku huo huku ikiripotiwa kuwa zaidi ya watu 30 wameuawa na zaidi ya watu 60 wamejeruhiwa vibaya.Polisi wa Kenya wamewaambia wananchi wasiende eneo hilo ambapo kikosi maalum cha jeshi la G.S.U.maarufu kama 'fanya fujo uone' kimepelekewa eneo hilo kuwasaka na kukabiliana na washambuliaji hao.

Hili ndilo jengo lililovamiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni