Timu zilizofuzu kombe la dunia Brazil 2014 hadi sasa.
Safari ya kuelekea kwenye michuano mikubwa kuliko yote katika mchezo wa soka ya Kombe la Dunia la FIFA imeanza kuiva .
Huku michezo ya kufuzu kwa michuano hiyo ikiwa ukingoni ikiwa
imesaliwa na raundi mbili za mechi kwa kila kanda tayari kuna mataifa ya
meshakata tiketi ya kucheza michuano hiyo baada ya kufuzu mapema huku
kukiwa na mechi kadhaa za kufuzu zimebakia .
Barani ulaya mataifa kama Ujerumani , Italia , na Uholanzi
zilifanikiwa kukata tiketi baada ya matokeo ya michezo yao ya jana
ambapo Ujerumani iliwafunga San Marino 3-0 . Italia walifuzu baada ya
kushinda kwa 2-1 dhidi ya jamhuri ya Czech na Uholanzi walikata tiketi
yao baada ya kuwafunga Andorra 2-0.
Barani Amerika ya kusini Argentina walifanikiwa kuwa timu ya kwanza
kwenye kanda ya CONMEBOL kufuzu baada ya kuwafunga Paraguay 5-2 huku
nahodha na nyota wa timu hiyo Lionel Messi akifunga mabao mawili .
Amerika ya Kaskazini ilishuhudia timu ya taifa ya Marekani ikifuzu
baada ya kuwafunga watani wao wa jadi Mexico 2-0 . Marekani wanaungana
na Costa Rica ambao watakuwa wanashiriki kombe la dunia kwa mara ya
kwanza tangu mwaka 2006 baada ya kufuzu kwa matokeo ya sare ya 2-2
katika mchezo dhidi ya Honduras.
Kabla ya jana timu toka ukanda wa bara la Asia kama Japan , Australia
,Iran na Korea ya Kusini tayari zilikuwa zimefuzu mapema huku mchakato
wa kufuzu wa bara hilo ukiisha mapema .
Barani Afrika mchakato wa kufuzu uko kwenye hatua zake za mwisho
ambapo timu kumi zimefuzu kwenye hatua ya mtoano itakayohusisha mechi
mbili nyumbani na ugenini zitakazotoa timu tano zitakazoiwakilisha
Afrika huko Brazil.
Timu za Ethiopia,Cape Verde,Egypt,Algeria,Nigeria , Ghana , Ivory
Coast,Cameroo,Senegal na Burkina Faso zitapangiwa mechi mbili ambazo
ratiba yake itapangwa jumatatu ijayo .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni