WAKATI Taifa likiwa katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ajali mbaya imetokea katika eneo la Kibwabwa barabara kuu ya Iringa - Mbeya baada ya basi la Sai- Baba Express kugongana uso kwa uso na lori la kampuni ya Ivori mchana wa leo.
Basi hilo la kampuni ya Sai - baba Express lenye namba za Usajili T 668 BCD ambalo liligongana uso kwa uso na lori la kampuni ya Ivori lenye namba T 280 ADK ndilo ambalo linatajwa kuwa chanzo cha ajali hiyo.
Mashuhuda wa ajali hiyo wameueleza mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 8 mchana wakati basi hilo likitokea mkoani Mbeya na Lori hilo likitokea mjini Iringa na hivyo kugongana uso kwa uso .
Mmoja kati ya abiria wa basi hilo Yusuph Juma alisema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa katika mwendo kasi mbali ya eneo hilo la mji kuwepo alama zinazokataza spindi zaidi ya 50 ila bado basi hilo lilikuwa katika mwendo zaidi .
Alisema kuwa mbali ya magari hayo kugongana uso kwa uso ila bado basi hilo liliweza kushindwa kusimama na kulazimika kusimama zaidi ya mita 200 kutoka eneo la ajali .
Hata hivyo alisema ni jambo la kushuruku Mungu katika ajali hiyo mbali ya dereva wa lori kujeruhiwa vibaya wengine waliojeruhiwa ni pamoja na utingo wa basi na abiria mmoja huku abiria wengine zaidi ya 50 wakinusurika katika ajali hiyo.
Viongozi mbali mbali wa jeshi la polisi ,Sumatra na mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Bw Salim Asas ni miongoni mwa mashuhuda waliofika kushuhudia tukio hilo ambalo limetokea huku taifa likiwa katika wiki ya nenda kwa usalama taifa yatakayodfanyika kitaifa jijini Mwanza kuanza wiki ijayo chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania . |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni