Social Icons

Ijumaa, 13 Septemba 2013

Maji yagunduliwa Turkana, Kenya

Eneo kavu la Turkana kaskazini mwa Kenya
Eneo kavu la Turkana kaskazini mwa Kenya
 
Wanasayansi wametangaza kupata chanzo kikubwa cha raslimali ya maji katika  eneo kavu na masikini sana la  Turkana  kaskazini  mwa Kenya.
Ugunduzi huo ulitangazwa Jumatano kufuatia utafiti wa teknolojia ya satellite uliofanywa na shirika la kimataifa la elimu na sayansi UNESCO kwa ushirikiano na serikali ya Kenya.

Utafiti huo uligundua mabwawa  mawili  makubwa na yenye maji mengi chini ya ardhi huko Turkana yakiwa na ukubwa  cubic mita bilioni 250 za maji  yanayokisiwa kuwa maradufu kiasi cha  maji Wakenya wanayotumia.  

Wanasayansi hao wanasema uchunguzi zaidi utafanywa kubaini  usalama wa maji hayo. Umoja wa Mataifa unasema Wakenya milioni 17 au asili mia 40  hawana maji safi ya kunywa.

Nao maafisa wa Kenya wamesema ugunduzi huo utasaidia serikali kuhudumia raia wa eneo la Turkana ambalo ni kavu pamoja na maeneo mengine ya nchi yenye utashi mkubwa wa maji.

Eneo la Turkana  limo kaskazini mwa Kenya na linapakana na Uganda, Sudan Kusini na Ethiopia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates