TATHMINI YA MAJINA KUTOKANA NA HERUFI ZA MWANZO ZA MAJINA HAYO
HERUFI A
Mwenye
jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa,
anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye
tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda
Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.
HERUFI B
wenye jina
linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi.
Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anap
otaka kulinda vilivyo katika himaya yake.
HERUFI C
Mwenye
jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika,
mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa
wabunifu na wanaopenda mawasiliano.
HERUFI D
Mwenye jina
linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu
wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.
HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye
roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi
na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na
kigeugeu.
HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu
mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni
mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.
HERUFI G
Mwenye
jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na
nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya
watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali
ushauri wa kutoka kwa watu.
HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia
na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida
kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi,
mchoyo na mbinafsi.
HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na
herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi
hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.
HERUFI J
Mwenye jina
linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na
muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati
mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.
HERUFI K
Mwenye
jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo
thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu
wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na
hali ya kimaisha.
HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L
ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa
wanapata ajali mara kwa mara.
HERUFI M
Mwenye jina
linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na
hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.
HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.
HERUFI O
Mwenye
jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye
bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo
mkubwa wa kudhibiti hisia.
HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia
na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu
za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.
HERUFI Q
Mwenye
jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni
watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata
hivyo ni mtu aliyepooza sana.
HERUFI R
Mwenye jina
linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana
hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.
HERUFI S
Mwenye
jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta
utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.
HERUFI T
Mwenye
jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho,
anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda
mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.
HERUFI U
Mwenye
jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla.
Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na
aliyekosa maamuzi.
HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.
HERUFI W
Mwenye
jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi
na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na
hufanya mambo ya hatari.
HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na
herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni
rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.
HERUFI Y
Mwenye
jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi
kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia
kupoteza bahati katika maisha.
HERUFI Z
Mwenye jina
linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni
wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo December 15, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam December 15,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za M...
Dakika 39 zilizopita
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni