Social Icons

Jumapili, 29 Septemba 2013


Miss Philippines avishwa taji la Miss World na miss kutoka Ghana awa mshindi tatu. Angalia picha ya tukio jinsi lilivyokuwa.

miss world
Miss Philippines  Megan Young mwenye umri wa miaka 23 amevishwa taji la Miss World ambalo limefanyika leo hii huko Indonesia. Megan ni mzaliwa wa Marekani na ana umri wa miaka 23 anasomea mambo ya digital film. Mshindi wa pili ametoka France na watatu kutoka Ghana.
Megan akitoa hotuba ya shukrani baada ya kuvishwa taji na Wenxia Yu wa China ambaye ndiyo Miss World aliyemaliza muda wake leo, Megan ameahidi kuwa miss world bora zaidi ya waliowahi kutokea.
995516_555633037824176_564996907_n
1382107_555683994485747_610847827_n (1)
559837_555611951159618_2054106488_n
1235462_555612107826269_1813106139_n
1375877_555695317817948_68335901_n
1379289_555682527819227_1871897359_n
1382163_555612087826271_124534911_n

MAKALA.

HIVI NDIVYO PANYA WANAVYOTUMIKA KUGUNDUA MABOMU ARDHINI

Shirika moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza kuwafundisha panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini. Panya hao ambao ni wakubwa kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa majaribio Morogoro Tanzania .Inaaminika wanauwezo mkubwa wa kunusa kuliko mbwa. Hii inatokana na kuwa pua zao zipo karibu na ardhi,hali ambayo inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu.


Panya wanafundishwa jinsi ya kunusa wakiwa wadogo, kwa kuwekewa vitu vyenye madini ya milipuko.Tangu mwaka 2000, APOPO imekuwa ikiwafunza panya kwenye chuo cha Sokoine,Morogoro. Mwaka 2006 panya wa hao walianza zoezi la kutafuta mabomu ya ardhini huko Msumbiji. Kabla ya panya kuanza kazi ya kunusa wapi mabomu yalipo, lazima wafuzu mtihani kutimiza viwango vya kimataifa vya kutambua mabomu ardhini.


Panya hujifunza kufuata eneo fulani hatua kwa hatua. Waya au kamba hufungwa mwilini kutoka kwenye ufito. Wasimamizi wawili husimama kila upande wa ufito na kumruhusu panya kutembea toka mwanzo wa ufito hadi upande mwingine kwa kufuata jinsi waya au kamba alizo fungwa mwilini. Katika mafunzo ya awali panya hufunzwa kunusa kemikali aina ya TNT ndani ya chombo cha chuma


Baadaye kila panya hufanya mafunzo kwenye eneo ambalo kuna mabomu ya ardhini yaliyofukiwa na vifaa ambayo huzuia mlipuko. Ikiwa panya ameweza kunusa na kutambua yalipo madini asilia ya TNT huwa anasimama na kuanza kufukua sehemu hiyo ya ardhi iliyofukiwa bomu. Kuwafundisha panya kunachukua muda wa mwaka na inagharimu dola za Kimarekani $6,000 sawa na Euro 4,670



Wakati wa mafunzo panya hupewa zawadi kwa kufuzu vizuri kwa sauti maalumu ambayo inaashiria kufuzu kwake na kupewa kipande cha ndizi kama zawadi. Panya aliyefuzu vizuri huwa ana uwezo wa kuzunguka mita 400 za mraba kwa siku, wakati eneo kama hili litamchukua binadamu wiki mbili ili kuweza kugundua wapi kumefukiwa bomu



Kulinganishwa na mbwa, panya wanaweza kutumiwa na mtu yeyote kwani hawana tabia ya kutokuwa na mahusiano ya karibu na mtu aliyemfundisha kama walivyo mbwa. Panya anaweza kufanya kazi ya kufichua mabomu, hata kama aliyemfundisha hayupo na huwa wanafanya kazi vizuri kwa ufanisi na mtu yeyote. Hakuna shida kwa panya aliyefundishwa Tanzania, kwenda kufanya kazi Msumbiji, Angola,Thailand na Kambodia



Hadi kufukia sasa nchini Msumbiji, zaidi ya mita za mraba milioni 6,5 za ardhi zimeshachunguzwa na mabomu 2,000 yaliyotegwa ardhini yamepatikana na kuharibiwa, pia bado mabomu 1,000 kuteguliwa na bunduki na silaha nyingine ndogo 12,000 zilipatikana. Na mpaka sasa kuna makundi saba yenye watu 54 ambayo yanashughulika na kazi ya kutegua mabomu kwa kuwatumia panya


HEBU ONA MAAJABU YA WANASAYANSI, WAMPANDIKIZA HUYU JAMAA PUA KWENYE PAJI LA USO

Xiaolian,      22, akiwa na pua mpya ‘iliyopandwa’ na madaktari katika paji lake la uso.
Mmoja wa madaktari walioendesha tiba hiyo akifanya tathmini ya kitaalam kwa Xiaolian.
RAIA mmoja wa nchini China anayejulikana kwa jina moja la Xiaolian, mwenye umri wa miaka 22, ametengenezewa pua nyingine na madaktari ambayo sasa imewekwa kwenye paji lake la uso, baada ya ile ya asili kuharibika katika ajali ya gari iliyomkumba Agosti, 2012. Madaktari wameitengeneza pua hiyo kwa kutumia sehemu mbalimbali za mwili wa mtu huyo zikiwemo sehemu za mbavu na ngozi yake. Operesheni hiyo imefanyika katika hospitali moja huko Fuzhou, katika Jimbo la Fujian. Wataalam hao wanatarajia kuihamisha pua hiyo na kuiweka sehemu ambapo pua yake ya zamani ilipokuwa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MSANII AHUKUMIWA MIEZI 6 KWA KUIMBA MATUSI

Msanii wa kizazi kipya nchini Tunisia, Ahmed Ben Ahmed, anayejulikana kwa jina la kiusanii, Klay BBJ, amehukumiwa jela kwa miezi sita kwa kuwatusi maafisa wakuu kupitia kwa muziki wake.
Mahakama ilitupilia mbali kesi yake ya rufaa baada ya yeye na mwanamuziki mwenzake kupatikana na hatia mwezi jana ya kuwatusi maafisa wakuu katika tamasha la muziki eneo la Hammamet.
Wawili hao awali walihukumiwa bila ya wao kuwepo mahakamani kutumikia kifungo cha miezi 21 lakini hukumu hiyo iliondolewa.
Weld El 15, aliyepatikana na kosa kwa kuimba wimbo wake huo, kuwa 'Ploisi ni Mbwa', hakukata rufaa na sasa yuko mbioni.
Hata hivyo Kaly BBJ lisema kuwa wimbo wao ulikuwa unaelezea hali ilivyo nchini Tunisia na kuhusu serikali.
Muungano wa vyama unaoongozwa na chama cha wanasiasa waisilamu wenye msimamo wa kadri, Ennahda, uliingia mamlakani baada ya mapinduzi ya kiraia yaliyomwondoa mamlakani aliyekuwa rais Zine el-Abidine Ben Ali mwezi Januari mwaka 2011 na uchaguzi kufanyika baadaye mwaka huo.
Klay anasemekana kuambia mahakama kuwa wimbo wao unakosoa hali ya sasa serikalini na kote nchini Tunisia tu.
Alisema yeye ni mmoja wa wanamuziki wanaokosoa sana serikali na ndio maana wamekuwa wakimsaka sana.
Lakini majaji walikataa rufaa aliyowasilisa na kusema hukumu yake ya miezi sita gerezani inastahili kuanza mara moja.
Wakili wake alisema kuwa watawasilisha rufaa nyingine kupinga hukumu dhidi yake.

Ijumaa, 27 Septemba 2013

SAKOLOJI

MAMBO 5 AMBAYO NI VYAZO VYA BAHATI MBAYA
“Alikuwa anavuka barabara, lakini kwa bahati mbaya akagongwa na gari.” “Nimemaliza masomo yangu mwaka jana, lakini kwa bahati mbaya nikafeli.” Kwa bahati mbaya biashara yangu ilisambaratika.” “Kwa bahati mbaya alifukuzwa kazi.” Imetokea kwa bahati mbaya” Nimebata bahati mbaya Mume wangu hanifai hata kidogo.” “Kwa bahati mbaya alijifungua mtoto aliyekufa”
 Hizi ni baadhi kauli za baadhi ya watu ambao ni wafuasi wakubwa wa kitu kinachoitwa bahati mbaya katika maisha yetu ya kila siku. Hebu tujifunze  vyanzo vya bahati mbaya na namna ya kuepukana nayo, ili tusijikute kila siku tunalaumu kupatwa na bahati mbaya kumbe makosa ni yetu na kwamba hatukuwa makini katika kuishi kwetu.

 UZEMBE WA KUFIKIRI
Watu wengi wanaoamini kuwepo kwa matukio ya bahati mbaya katika maisha wanaelezwa na wataalamu kuwa na kasoro katika upeo wa kufikiri vyanzo vya mambo. Inasemwa na watafiti wengi kuwa matukio mabaya yaliyopata kuripotiwa ulimwenguni ni matokeo ya uzembe wa kufikiri na kuamua. Kwa maana hivyo inashauriwa kuwa mtu anayetaka kuepukana na bahati mbaya lazima awe hai katika fikra, hasa upataji wa jibu la mapema juu ya nini kitatokea katika kutenda kwake.
 Inampasa mvuka barabara kwa mfano, ajiuliuze matokeo ya kuvuka kwake na apate majibu chanya na hasi na ahakiki matokeo hasi ambayo kwa kawaida ndiyo yenye madhara. Vivyo hivyo kwa dereva anayeendesha chombo cha moto, msichana anayetaka kuolewa, mfanyabiashara, mfanyakazi, anayefanya mapenzi, anayesoma, wote kwa ujumla wao lazima wawe na majibu ya kwa nini wanataka/ wanafanya hayo, kisha wajadili akilini matokeo mabaya ambayo yapo na kuyatafutie njia ya kuepukana nayo.

 KUTOTUMIA UWEZO WOTE
Mwanadamu natajwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo kuliko wengi wao wanavyodhani. Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kuwa asilimia 70 ya watu ulimwenguni, hasa wale wa dunia ya tatu wanaishi chini ya uwezo na vipaji walivyonavyona. Kwa kuzingatiahilo wahanga wengi wa bahati mbaya ni wale ambao hawatumii uwezo wao wote au zaidi ya nusu ya vipaji vyao katika kupambana na matokeo mabaya.
  Wanafunzi wengi hawasomi kwa uwezo wao wote, wataalamu, wanasiasa, viongozi, watendaji hawatumii uwezo wao wote kufanya kazi na majukumu waliyonayo, matokeo yake wanalipua kazi na baadaye kuleta matokeo mabaya kisha kuyapa jina la BAHATI MBAYA. Inasemwa kuwa kila mahali palipo na janga msingi wa kwanza kutazamwa kwa watu wenye uelewa ni UZEMBE na kutotumika kwa uwezo halisi wa wahusika katika kukinga matokeo mabaya.

 KUAMINI VIASHIRIA VYA KUSHINDWA
 Kuna watu ambao hupatwa na matokeo ya bahati mbaya baada ya kuamini viashiria vya kushindwa na kuacha kujizatiti katika nguvu za ushindi. Kwa mfano timu ya mpira inaweza kufungwa magoli 3 kipindi cha kwanza, matokeo hayo yakiaminiwa na wachezaji yanaweza kunyonya nguvu ya ushindani na kuikaribisha bahati mbaya, kumbe wangepuuza viashiria hivyo vya kushindwa mapema wakaongeza nguvu wangeweza kurudisha na pengine kushinda mchezo.
  Vivyo hivyo, tunapokuwa tunafanya jambo fulani, kuna viashiria vinaweza kujitokeza kututia hofu kwamba tutashindwa, tunashauriwa kutokata tamaa. Kama wewe ni muuguzi umemuona mgonjwa wako anashindwa kupumua usipunguze harakati za kumtibu kwa kuamini viashiria kwamba anakufa muda mfupi ujao, badala yake zidisha juhudi za kumuokoa. Mfanyabiasha pia ukiona biashara inayumba usikate tamaa, ongeza bidii kwa kufanya hivyo utakuwa unapambana na bahati mbaya na kwa mujibu wa wanasaikolojia utakuwa umenyonya nguvu za mabaya na hivyo kutokukupata.

KUYUMBA KATIKA MAAMUZI
 Kuna watu ambao kwa hakika kabisa wanaweza kuwa wamefikiri vema, wametumia uwezo wao wote, hawakuamini viashiria, lakini wakajikuta wanapatwa na bahati mbaya kwa kuyumba katika maamuzi, hasa wakati wa kuhitimisha jambo fulani.
  Kwa mfano mtu anaweza kuwa ametafuta mchumba, akamhakiki kama nilivyosema, lakini likatokea neno la umbea fulani likamyumbisha na akajikuta amemwacha mchumba wake na kuchukua mwingine ambaye hakumhakiki katika fikra. Inashauri kwamba mtu asiyumbe katika maamuzi sahihi aliyoyathibitisha.

 KUMBUKUMBU MBAYA
 Katika maisha yetu kuna watu wengi ambao wanasogeza bahati mbaya kwa kujaza kumbukumbu mbaya za matukio hasi kwenye akili zao. Wapo mahodari wa kukumbuka mahali zilipotokea ajali za magari, yaani wakifika hapo tu mioyo inakwenda mbio. Kuna wanaokumbuka rafiki zao waliokufa wakati wanajifungua na wengine wana historia za nani alipatwa na mabaya baada ya kufanya jambo fulani na wengine wanawafahamu kwa majina waliokufa bila kuzaa, yote hayo ni kujitia hofu tupu.
 Kuishi na wingi wa kumbukumbu mbaya ni kosa kubwa kwani hutengeneza uzembe wa mwili ambao huleta matokeo mabaya bila mhusika kujijua. Ndiyo maana unaweza kukuta ajali nyingi hutokea zaidi eneo moja kutokana na madereva wapitao hapo kujaza kumbukumbu mbaya ambazo huwaondolea umakini. Hivyo kama tunataka kuepukana na bahati mbaya ni vema tukaondoa kumbukumbu mbaya zinazotia hofu na hata kama tutakumbuka iwe kwa ajili ya kuongeza umakini na isiwe kwa kupata woga wa kuvuka salama eneo au tukio hilo.


Sehemu ya jengo la Westgate iliyoporomoka

Wakuu wa usalama kuhojiwa Kenya


Sehemu ya jengo la Westgate iliyoporomoka
Maafisa wakuu wa ujasusi wametakiwa kufika mbele ya kamati ya ulinzi ya bunge ili kuhojiwa kuhusu mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jumba la Westgate mjini Nairobi.
Taarifa kwenye vyombo vya habari nchini humo zinaonyesha kuwa hali ya kulaumiana imeanza kuibuka huku mashirika ya usalama yakinyosheana kidole.

Wataalamu wa uchunguzi wa mauaji wangali wanafanya uchunguzi wao wakitafuta miili na dalili za kilichosababisha shambulizi hilo.Watu 67 waliuawa kwenye shambulizi hilo huku zaidi ya miamoja sabini na tano wakipata majeraha mabaya. Shirika la Red Cross nalo linasema kuwa watu 61 wangali hawajulikani waliko.

Kamati ya bunge inataka maafisa wanaohusika na maswala ya usalama waweze kuwajibishwa.
Kundi la kigaidi la nchini Somalia, al-Shabab limedai kufanya mashambulizi hayo yaliyodumu siku nne kama hatua ya kulipiza kisasi kwa Kenya kujihusisha nchini Somalia kijeshi.
Hii leo ni siku ya tatu ya maombolezi kwa wathiriwa wa shambulizi hilo wakiwemo raia na wanajeshi.
Rais Uhuru Kenyatta amehudhuria mazishi ya mpwa wake na mchumba wake mjini Nairobi ambapo aliwahutubia waumini.

Walipuuza onyo?

Hatua ya kuwataka maafisa hao wa usalama kufika mbele ya tume ya bunge siku ya Jumatatu, inakuja kutokana na wasiwasi miongoni mwa wakenya kuhusu kiwango cha maafisa hao kujiandaa kwa tukio lolote la kigaidi sawa na lililotokea Westgate.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mmoja wa maafisa waliotakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ni mkuu wa shirika la ujasusi Michael Gichangi, anayesema alitoa taarifa za ujasusi kuhusu shambulizi hilo kwa polisi.
Lakini, afisaa mmoja mkuu katika idara ya polisi alikana kuwa taarifa hiyo ilitolewa kwa polisi.

Alhamisi, 26 Septemba 2013

MAKALA



Al Shaabab Ni Nani?

ULIMWENGU umepatwa na mshtuko mkubwa kwa kuona picha za tukio kubwa la kigaidi kwenye moja ya maduka makubwa jijini Nairobi. Hili ni shambulio kubwa la kigaidi kupata kutokea Afrika Mashariki tangu lile la mwaka 1998. Na ajabu ya kihitoria ni kuwa matukio mengi ya kigaidi yametokea katika mwezi wa Septemba.

La Nairobi ni shambulizi la kigaidi la kulaaniwa vikali na wapenda amani wote ulimwenguni. Hata hivyo, moja ya tafsiri ya vitendo vya kigaidi tunavyovishuhudia Nairobi ni kuwepo kwa hali ya vita vya kigaidi vyenye kuendeshwa kwenye maeneo ya mijini (Urban terrorism).

Ni shambulizi lenye athari mbaya kiuchumi si tu kwa nchi ya Kenya, bali hata majirani zake ikiwemo Tanzania. Ni shambulizi lililowaogopesha wageni wengi wakiwamo wawekezaji pia. Kwamba Al Shabaab inalenga pia nchi za Magharibi. Hivyo basi, hata raia wake. Kunahitajika jitihada za pamoja kuwaondoa hofu watu wa mataifa ya nje, kuwa kilichotokea Nairobi kitadhibitiwa kwa njia zote, kisitokee tena.
Na hakika, aina hii ya ugaidi ni ngumu sana kudhibitika hatakama nchi ina jeshi kubwa na lenye vifaa vya kisasa. Inahitaji ushiriki wa raia wema katika kutoa taarifa za wahalifu hata kabla hawajafanya matendo yao maovu. Inahitaji pia maandalizi makini, ya kuwa na vikosi vilivyo tayari wakati wote kukabiliana na matukio kama haya.

Ni dhahiri, kuwa mbinu inazotumika kikundi cha kigaidi cha Al Shaabab ambacho maana hasa ya jina hilo ni ' Vijana', ni moja ya changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Al Shabaab iliundwa mwaka 2006. Kinasemekana kuwa na wapiganaji wenye silaha wapatao 10,000. Al Shabaab katika miaka ya karibuni wamepoteza maeneo mengi ya mijini waliyokuwa wakiyadhibiti, ikiwamo mji wa Kismayu ambao majeshi ya Kenya yaliudhibiti baada ya kuwasambaratisha Al Shabaab. Kwa sasa Al Shabaab bado wana nguvu maeneo ya vijijini katika Somalia.

Kufuatia Kenya kujiingisha kijeshi kupanbana na Al Shaabab, kikundi hicho kimeifanya Kenya kuwa adui na kutangaza wazi azma yake ya kuishambulia Kenya. Mwezi Aprili mwaka huu watu watano walipoteza maisha nchini Kenya baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kuingia kwa nguvu wakiwa na silaha kwenye mgahawa mmoja kwenye mji wa Garissa nchini Kenya.

Mwaka 2012 ndipo Al Shabaab walipojiunga rasmi na mtandao wa kigaidi wa Al qaida chini ya kiongozi wa Al qiada, Ayman al- Zawahiri.
Hakika, hapa duniani matukio ya kigaidi yameongezeka.
Kwa faida ya wasomaji, nitaanza kwa kuangalia chimbuko la ugaidi kihistoria. Ni rahisi kusema kwamba ulimwengu umebadilika baada ya ugaidi wa Septemba 11 mwaka 2001 kule Marekani. Kwamba ugaidi umesogea karibu zaidi katika fikra zetu. Watanzania bado tunakumbuka tukio la shambulizi la kigaidi dhidi ya jengo la Ubalozi wa Marekani jijini Dar Es Salaam Agosti 7, 1998.

Sura ya ugaidi imeonekana vema zaidi miongoni mwa walimwengu. Bila shaka, picha ya filamu ya televisheni yenye kuonesha majengo mawili ya World Trade Centre kule Marekani yakitunguliwa na kuanguka, zimeonwa na takribani asilimia 75 ya watu wa ulimwengu huu. Katika hili la kuchambua ugaidi, hebu
basi tuanze na kujiuliza; Ugaidi ni nini?

Itakumbukwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano walipokutana Dodoma mwaka 2002 walipitisha Muswaada wa Ugaidi. Wabunge wetu walitumia muda mwingi sana kujadili tafsiri ya neno "ugaidi".
Kwa kifupi, ugaidi ukitafsiri kutoka neno la Kiingereza "Terrorism" tunapata maana ya "hofu". Neno la Kiingereza "Terror" lina maana ya hali ya "kutisha".

Vitendo vya kigaidi hutumiwa na mtu au makundi ya watu ili kuwaingizia watu hofu ndani ya mioyo yao na pengine hata kuchukua madaraka ya kisiasa. Ugaidi ni njia ya mnyonge na hata mwenye nguvu kutimiza malengo yake. Hili litafafanulika zaidi kadri utakapofuatilia maandiko haya.

Kihistoria tunaona kuwa, vitendo vingi vya kigaidi humu duniani vimefanywa pia na dola zilizo madarakani kwa minajili ya kuendelea kushika hatamu za dola. Mathalan, msemo wa " Utawala dhalimu" kwa tafsiri ya Kiingereza "Terror regime" hutumika tunapoielezea dola yenye kutumia mabavu na nguvu nyingi kupita kiasi. Dola au mtawala asiyezingatia sheria wala haki za kibinadamu.

Msamiati huu wa utawala dhalimu unatokana na lugha ya Kifaransa na una chimbuko la Mapinduzi ya Wananchi kule Ufaransa kati ya mwaka 1789 hadi 1799. Utawala dhalimu wenye kutisha" la terreur" ulikuwepo kule Ufaransa kunako miaka ya kati ya 1792 hadi 1794. Katika kipindi hicho watu takribani 40,000, wengi wao wakiwa wakulima na wahunzi waliuawa.

Mifano ya tawala dhalimu na za kutisha katika sehemu nyingine za dunia ni kama Urusi ya zamani chini ya dikteta Stalin, utawala wa Kinazi wa Ujerumani kati ya 1933-1945 chini ya Fashisti Hittler.
Katika Afrika, tuna pia mifano kadhaa ya tawala dhalimu na za kutisha ambazo kimsingi ni tawala za kigaidi. Uganda ya Idd Amin, Afrika ya Kati ya Bokassa, Zaire ya Mobutu, na nchi nyingine nyingi. Hizi zilikuwa tawala dhalimu.

Ugaidi kimsingi ni ile hali ya mtu, kikundi au dola, kwa maana ya taifa,kutumia nguvu nje ya wigo wa sheria ili kufikia malengo yao. Mwenye kuendesha vitendo vya kigaidi huchagua watu wake watakaoathirika na vitendo hivyo. Si lazima mtu au watu hao watakaoathirika wawe ni wahusika wa moja kwa moja wa mgogoro husika, isipokuwa, waathirika mara nyingi huchaguliwa na huonekana kama wawakilishi wa malengo ambayo magaidi wanataka kuyafikia.

Malengo au sababu za ugaidi zaweza kuwa ni za kidini, kijamii na kisiasa.
Ugaidi huwa wa kimataifa pale tukio la kigaidi linapofanywa nje ya mipakaya yule anayatenda tendo la kigaidi, au raia wa nchi moja wanapokuwawalengwa na kauthirika na tendo la kigaidi katika nchi ya tatu, mathalan,magaidi kutoka Colombia wanapofanya tendo la kigaidi dhidi ya raia waUingereza katika nchi ya Zambia.

HUU NDIO UWANJA WA TAIFA WA SOKA WA SOMALIA UNAVYOONEKANA

https://scontent-b-vie.xx.fbcdn.net/hphotos-ash3/q71/532078_631757903511063_496276965_n.jpgUwanja wa Soka wa Taifa wa Somalia unavyoonekana kwa sasa. Kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab kimepiga marufuku soka kuchezwa kwenye Uwanja huo na sehemu nyingine yoyote ya Mogadishu tangu mwaka 2008. Serikali ya Somalia juzi imeingia mkataba na kampuni ya moja ya China
kukarabati miundombinu ya Uwanja huo lakini imeripotiwa kwamba kampuni hiyo inaogopa kushambuliwa na inasita kuanza kazi.

Jumatano, 25 Septemba 2013


Upinzani ‘wawasha moto’ Zanzibar,wataka Chikawe ajiuzulu kwa taarifa za uongo.

Waziri wa Sheria na Katiba Mathias Chikawe ametakiwa ajiuzulu kwa kutoa taarifa za uongo kwamba Zanzibar ilishirikishwa kabla ya Muswada wa Mabadiliko ya Katiba kuwasilishwa bungeni na kupitishwa na Bunge Septemba mwaka huu.
Msimamo huo ulitolewa na Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar, Aboubakary Khamis Bakari wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliovishirikishwa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi uliofanyika Uwanja wa Kibandamaiti mjini Unguja jana.
Aboubakari alisema kwamba Zanzibar ilipokea taarifa ya awali ya mabadiliko kuhusu vifungu vinne vya Muswada wa Mabadiliko ya Katiba na kutakiwa Zanzibar itoe maoni na mapendekezo yake, jambo ambalo alisema lilifanyika kupitia Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hata hivyo, alisema vifungu vya mabadiliko ghafla viliongezwa kutoka vinne hadi 12 bila ya Zanzibar kupewa nafasi ya kujadili vifungu vinane ambavyo vina umuhimu mkubwa katika kupata katiba bora.
“Waziri nimesoma naye Chuo Kikuu mwaka 1972, Chikawe kwa hili amesema uongo vinginevyo ajiuzulu, hafai,” alisema Aboubakari.
Alisema kabla ya kufanyika Waziri akifuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, William Lukuvi walifika Zanzibar na kutaka wajadili vifungu hivyo kwa siku moja jambo ambalo alipinga kulitekeleza.
“Baada ya kuanza kupiga kelele, wenzetu walikuja Zanzibar wakitaka tujadili mabadiliko ya mswada,nikawaambia siwezi kujadili masilahi ya nchi kijuujuu, huko ni kuiuza nchi, siko tayari kufanya hilo,” alisema.
Aboubakari alisema marekebisho yaliyofanyika katika muswada huo na kutoa nafasi kujadili na kupitisha mabadiliko ya Katiba kwa kutumia wingi wa kura ni sawa na wazimu.
Alisema mabadiliko yoyote ya Katiba yanapaswa kutumia theluthi mbili toka pande mbili za Muungano, utaratibu ambao ndiyo umekuwa ukitumika na nchi mbalimbali zenye mfumo kama wa Tanzania. Mwananchi ilipomtafuta Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kujibu tuhuma hizo alisema Aboubakari ameudanganya umma mchana kweupe kwa vile yeye na Waziri Lukuvi walifika Zanzibar kupeleka rasimu ya muswada na si kujadili na kupokea mapendekezo papo kwa hapo.
Chikawe alisema kwamba walipokabidhi muswada pia walimtaarifu siku ya kuwasilishwa muswada huo katika kikao cha Bunge na kuwataka kutoa maoni na mapendekezo kwa wakati mwafaka kabla ya kujadiliwa na kamati ya Katiba ya Sheria ya Bunge.
Alisema kwamba nyongeza ya marekebisho ya vifungu vinane yalitokana na mapendekezo ya wabunge katika kamati na michango ya wabunge ndani ya Bunge katika utaratibu unaoruhusiwa kisheria.
“Baada ya kamati ya Bunge kukaa, Mbunge Halima Mdee wa Chadema ndiye aliyependekeza kutumika kwa utaratibu wa wingi wa kura katika kupitisha mabadiliko hayo ya Katiba kama hatua ya theluthi mbili itashindwa kufikia mwafaka,” alisema Chikawe.Pia alisema mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi, Jaku Hashim Jaku yeye alitetea kwa nguvu ya hoja kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba imalize kazi yake baada ya kuwasilisha ripoti yake kwa Rais na kwamba haikuwa ni uamuzi na matakwa ya Serikali kama inavyodaiwa na vyama vya upinzani kuhusu nyongeza hiyo.
“Nyongeza ya vifungu ilitokana na wabunge katika kamati na ndani ya Bunge lenyewe, Serikali haiwezi kupuuzia ushauri wa wawakilishi wa wananchi na wabunge ambao wanaisimamia Serikali,” alisema Waziri Chikawe.
Aidha, Aboubakari alimshutumu Naibu Spika wa Bunge,Job Ndugai kwa kulidanganya Bunge kwa kitendo chake cha kutoa barua ikithibitisha Zanzibar imeshiriki wakati kuna vifungu vya ziada vimefanyiwa marekebisho bila ya kupata baraka ya Zanzibar.
Alisema kwa msingi huo amevunja na kukiuka kanuni za Bunge na wabunge wana haki ya kumshtaki kwa kutumia kanuni zao kwa kupotosha Bunge na umma.
Hata hivyo, taarifa hizo za Aboubakari kutokana na maelezo aliyotoa awali Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwenye mkutano wa hadhara, alisema Zanzibar ilishirikishwa katika kuvifanyia vifungu sita na SMZ ilitoa mapendekezo katika vifungu vitatu na baadae vikaongezwa vinane kinyemela bila ya Zanzibar kushirikishwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema kwa muda mrefu viongozi wa Zanzibar walikuwa wakijitolea kupigania mabadiliko ya taifa lao na kukutwa na vizingiti ikiwemo kuwekwa vizuizini na kupewa hongo ya madaraka.
Mbatia alisema miongoni mwa viongozi waliojitoa muhanga kutaka mabadiliko ya mfumo wa Muungano ni pamoja na Rais wa Awamu ya Pili Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi ambaye aliondolewa kibabe madarakani chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere.
Naye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimtaka Rais Jakaya Kikwete kumfuta kazi Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kwa madai kuwa hawana nia njema wakikusudia kuharibu nia njema ya Rais ya kupata Katiba mpya.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema Katiba iliyopo sasa nchini haifai kwa kuwa imejaa upungufu unaokwenda kinyume na misingi ya haki za raia.

VIONGOZI WA UPINZANI WAWASILI ZANZIBAR TAYARI KWA MKUTANO


 
 
Blogger Templates