Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amewaomba wapiga kura kukataa masharti ya wakopeshaji wa nchi hiyo wakati wa kura ya maoni hapo Jumapili.
Bw Tsipras amesema kwa kupinga kubana matumizi, Ugiriki itaweza kushauriana zaidi na kupata suluhu la mozozo wa sasa wa kifedha.
Siku ya mwisho kwa Ugiriki kugharamia madeni yake ni Jumanne wiki hii ambapo inatakiwa kulipa deni la Euro bilioni 1.6, kwa shirika la fedha duniani{IMF}.
Viongozi wa Muungano wa Ulaya wameonya hatua ya kukataa kulipa madeni yake ni sawa na Ugiriki kujiondoa kutoka kanda inayotumia sarafu ya Euro.
Hata hivyo Waziri Mkuu Tsipras amesema hataki nchi yake kuitema Euro.Mazungumzo kati ya Ugiriki na wakopeshaji wake yalivunjika wiki jana, hatua iliyosababisha benki za nchi hiyo kufungwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni