Balozi wa Burundi kwenye umoja wa mataifa amesema kuwa uchaguzi utaendelea jinsi ulivyopangwa siku ya jumatatu licha ya ombi kutaka uahirishwe kutoka kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon.
Ban anasema kuwa ana wasiwasi kuhusu hali ya usalama nchini Burundi kufuatia mzozo wa kisiasa unaoendelea huko.
Balozi Albert Shingiro aliuambia mkutano wa usalama wa umoja wa mataifa kuwa watu wanataka uchaguzi ufanyike.
Vyama vya upinzani na mashirika yasiyokuwa ya serikali tayari yametangaza kuwa watasusia uchaguzi huo.
Waandamanaji wanapinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania urais kwa muhula wa tatu wakidai kuwa inakiuka katiba ya Nvhi hiyo.
Rais Nkurunziza naye anashikilia kuwa awamu ya kwanza aliteuliwa na wajumbe wala sio raia kama vile inavyohitajika kwenye katiba iliyoundwa baada ya makubaliano ya Arusha yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenye nchini humo.
Takriban watu 50 wameuawa nchini Burundi tangu mwezi Aprili mwaka huu wakati rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwa atawania muhula wa tatu.
Maelfu ya raia wengine wa Burundi nao wamehamia mataifa jirani kwa hofu ya kuzuka mamchafuko zaidi.
Uchaguzi wa ubunge unatarajiwa siku ya Jumatatu huku uchaguzi wa urais ukipangiwa kufanyika tarehe 15 Julai mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni