Bondia wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya Mohammed Abdullah Kent ametoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kukutana na baadhi ya mabondia walioiwakilisha Kenya hapo awali.
Kent aliyewakilisha Kenya kuanzia mwaka 1973 hadi 1986 amesema kwamba kiongozi wa taifa alimuahidi kukutana nao lakini hajatizimiza ahadi hiyo kufikia sasa.
''Rais mwenyewe alisema anataka tukutane sana atusikize mambo yetu lakini najua ana shughuli zake nyingi za kitaifa. Naomba asisahau kupanga siku tukutane naye sisi mabondia wa zamani,'' alisema Kent
Amemtaka rais Kenyatta kuingilia kati na kuhakikisha kuwa anarudishiwa kipande chake cha ardhi alichopewa na rais mstaafu Daniel Arap Moi katika eneo la Mathare North 1983 ambacho alipokonywa na wanasiasa.
''Mabondia wameiletea Kenya sifa kubwa lakini tumesahauliwa. Katika michezo ya Olympiki ni mabondia na wanariadha tu ambao wameipatia Kenya medali'',aliongezea Kent.
Mbali na Kent na Muchoki, baadhi ya mabondia wengine ambao wako kwenye kundi hilo linalopanga kukutana na Rais Kenyatta ni George ''Mosquito'' Findo, Philip Waruinge na nduguye Sammy Mbogwa, Stephen Thega, Dick ''Tiger'' Murunga, Mike Irungu, Kamau Wanyoike, Isaiah Ikhoni, Aggrey Mwambi, Patrick ''Mont'' Waweru, David Makumba, Stephen ''Vedo'' Okumu, Ibrahim ''Surf'' Bilali, Omar Ahmed ''Kasongo'' na Suleiman Bilali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni